Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu, akijaribu kuwasha moja ya Pikipiki 16 zilizokabidhiwa kwa Polisi kama ishara ya kuzizindua kuanza kazi rasmi ya kupambana na uharifu mkoani Ruvuma. Pikipiki hizo zimetolewa na IGP Said Mwema, kwa madhumuni ya kusaidia usafiri Polisi jamii na kupambana na uhalifu. Pichani katikati anayeangalia kwa Makini ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki na Kulia anayetabasamu ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mhe. Charles Mhagama ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Matogoro.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Mjini Songea, ilifuatia kutolewa agizo kwa waendesha Pikipiki wote maarufu kama Yeboyebo hapa mkoani Ruvuma wa kufanya biashara ya kusafirisha abiria kuwa ni saa Sita Usiku. kila siku. Zaidi ya muda huo ni kuvunja amri halali ya serikali na kuto tii sheria kwa hiari.
Agizo hili linakuja kuokoa maisha ya waendesha Yeboyebo wanaouawa au kuporwa pikipiki zao.
(Picha kwa Hisani ya Muhidin Amri-Ndolanga)