Pages

Saturday, September 15, 2012

Jua Kali hadi mifukoni hapa Songea



Hakika hali ya uchumi hapa Songea waweza kuiona sehemu za masoko na hasa katika vitoweo.


"...jua kali hadi mifukoni." Wengi wanalia.

Hapa nilikuwa napita mitaa mbalimbali nikatokea eneo la Soko kuu la Songea pale wanawake wanapouza samaki wa kutoka Ziwa Nyasa ambalo linamzozo wa Mpaka Kati ya Tanzania na Malawi,

Samaki aina ya Mbasa, Mbufu, Mbelele na dagaa wale wadogo wa dogo na wakubwa ni maarufu sana, wanauzwa chini tu bila kujali, (Picha inajieleza)

Watamu, wanapendwa.

Nilisimamisha Gari eneo la Magharibi ya Soko Kuu la Songea amabako kuna mlango mdogo wa kutokea maarufu kwa kuuza samaki na dagaa kwa muda wa nusu saa sikuona mteja kuulizia samaki hao, Mama aliyekuwa akiuza kajifunika tu na Mwamvuli.

Mifuko ya wanunuzi nayo imepigwa na jua.

Haina miamvuli .

3 comments:

  1. Mwenga kaka Nyumayo mboni ukuninogesa sana somba Mbasa, Mbufu, Mbelele na dagaa haya bwana. Duh jua kali kiasi hiki ..

    ReplyDelete
  2. Mwenga Dada Yasinta, Somba Somba za Kunyanja na Ugali wa mayau......!

    ReplyDelete