Pages
▼
Wednesday, August 22, 2012
SIKU SABA GAZETI LA MWANAHALISI KUWA HURU?
WANAHARAKATI SALAAM!
Hatua zilizochukuliwa jana za kuitaka serikali ilifungulie Gazeti la Mwanahalisi na kuipatia siku saba kufanya hivyo, tunaziunga mkono kwa dhati.
Mwanahalisi lifunguliwe hata kabla ya hizo siku saba.
Waswahili husema Muungwana akivuliwa ngua, huchutama.
Serikali ilitakiwa ichutame, kwa kutolifungia Gazeti la Mwanahalisi lililosaidia walao serikali iwatambue watakaosaidia kuwakamata watuhumiwa.
Ndio uungwana. Serikali sikivu italitekeleza hili, haitataka kutunisha misuli kwa jambo kama hili. Viongozi watambue jukwaa pekee wakishatemwa madarakani ni kwenye vyombo vya habari. wasivibane, wanajibana wenyewe.
www.ruvumapress.blogspot.com
TANZANIA KWANZA
Niliwaza wazo, lakini wazo nililowaza sikuwaza nilivyowaza ntawaza, nimewaza wazo jingine kabisaa KWANI Ushabiki ,,,,fikra ,,,,Mtazamo,,,,Mawazo,,,yasifanywe ndiyo hoja za chuki,,,
ReplyDelete