Tuesday, September 10, 2013

WAANDISHI NA VINGOZI WA SERIKALI

Baadhi ya Waandishi wa habari wanaume wa mkoa wa Ruvuma, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya Mkoa wa Ruvuma. (Mwenye shati la maua katikati) ni  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabith Mwambungu ( jirani yake kushoto )  ni Mkuu wa Wilaya ya Songea,  Bw. Joseph Joseph Mkirikiti . ( Picha kwa hisani ya Ruvuma Press Club)

MTIHANI WA DARASA LA VII - 2013

Tunawatakia wanafunzi wote wa Darasa la Saba (VII) nchini mtihani mwema wa kumaliza elimu ya Msingi. utakaoanza kesho Jumatano 11, September 2013.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa
Mtihani huu utakaofanyika kesho ndio msingi imara utakao amua kuendelea na masomo ya sekondari kwa mwanafunzi muhusika au la.
Miaka hii ya karibuni, tumeshuhudia waziwazi vyombo vyetu vya usalama vimewakamata baadhi ya wanafunzi, walimu na mara nyingine hata wazazi kushiriki kikamilifu katika uhalifu wa kielimu wa kuiba mitihani .
Uhalifu huu unafanywa ili kuwafaulisha wanafunzi wasiostahili na ndio wanaokuwa mizigo katika elimu yao ya upili. Jambo hilo ni baya kupita maelezo kwani elimu ni sawa na moto. Moto haukopeshi, ukiweka mkono katika kaa la moto utaungua mara moja. Na elimu hali kadhalika kama kijana hana uwezo akapitishwa kwa hila kuendelea na masomo, huwa ni mzigo kwa kijana huyo, familia yake pia taifa.
Tusishangae kuona madaktari feki, wahandisi kanjanja, walimu mizigo wanasiasa bomu na wengine kibao bila kusahau wakulima wasiozingatia kanuni za kilimo bora.
Lengo kuu hapa ni kuwatakia mtihani mwema, usio na hila za kuvujishwa wala kuvujisha.
Jamii ya wanaRuvuma inasema hakuna linaloshindikana, utavuna ulichopanda.
Mtihani Mwema 2013

Saturday, August 31, 2013

KISOMO MWANZA WAPETA

Na Juma Nyumayo, Songea
KITUO Cha Taifa Kisomo Mwanza kinaendelea kutoa huduma zake kwa kuzingatia Matokeo Makubwa sasa (Big result Now) Kituo hiki kinaongozwa na Naibu Mkurugenzi Kisomo Mwanza, Bibi Mary Salu ambaye amewakaribisha wakuu wa vituo vya uchapaji kanda vya Songea, Mbeya, Tabora na Mkuu wa Press 'A' Dar es Salaam. angalia Picha zifuatazo.
Watumishi wa Kituo cha Kisomo Mwanza wakiwa katika Idara ya Computer, anayeonekana mbele ni Rabeca Fred akiwa kazini.



Mr Andrew Kingu akionyesha Ubora wa kazi zinazochapwa na Kiwanda cha Kisomo Mwanza

Naibu Mkurugenzi Kituo cha  Taifa Kisomo Mwanza, Bibi mary salu ( kushoto) akitoa maelezo kuhusu kiwanda cha uchapaji kisomo mwanza (kulia) ni juma Nyumayo toka Tujifunze Songea.



Friday, August 16, 2013

WAANDISHI WA HABARI RUVUMA WAONYWA

Na Steven Augustino, Songea
WAANDISHI wa Habari Mkoani Ruvuma wameonywa kuamini habari kutoka
mitandao na kuzitumia kuhabarisha umma bila  kuzifanyia utafiti wa
kutosha katika internet na kutumia vyanzo vya kuaminika ikiwemo
kuwahoji wahusika kupata habari za ukweli ambazo zitakuwa na manufaa
kwa wasomaji.
Hayo yameelezwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya
kuandika Habari kwa kutumia mitandao ya Internet na kutuma picha za
kihabari  Mtandaoni yanayoendeshwa katika Ukumbi wa Veta,Manispaa ya
Songea, Taasisi ya Vyombo vya habari kusini mwa Africa (Media
Institute of Southern Africa) MISA TANZANIA.
Wanahabari hao pia wanafundishwa namna ya kufanya utafiti wa vyanzo
vya habari mbalimbali katika Internet na kufungua njia nyingine za
mawasiliano kama  ‘youtube’, Blogu na namna ya kuzitumia katika tasnia
ya kutengeneza na kutuma habari zikiwa na takwimu sahihi.
Awali akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu, Afisa
Habari MISA -TANZANIA , Sengiyuva Gasiligwa,  alisema kuwa lengo la
mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kwenda na
wakati hasa katika teknolojia ya kimtandao.
Wanahabari hao pia wananolewa ili waweze kujua kwa undani maana ya
internet, ‘Worid Wide Web’ , ‘Computer’,  na matumizi yake kwa manufaa
ya maendeleo ya technolojia, uchumi, siaa na utamaduni na kujali
maadili
Gasiligwa alisema kuwa mafunzo hayo yanayo wahusisha Waandishi wa
Habari za Magazeti, Terevissin na Radio yanafanyika kwa ushirikiano
MISATAN na shirika la VIKES  toka Finland na kwamba kwa kuanzia
mafunzo hayo yalifanyika Mkoani Pemba huku Zanzibar Tanzania Visiwani
na sasa Ruvuma na baadaye mkoani mwanza.
Nae mwezeshaji wa mafunzo hayo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini
Iringa,  Saimon Berege,  pamoja na mambo mengine aliwataka Wanahabari
hao kuwa na ari ya kujiendeleza kielimu na kuwakaribisha kwenda kusoma
digrii ya pili (masters) Inayotolewa na chuo hicho.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wanahabari hao pamoja na kuipongeza
taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari
wamesema kuanzia sasa wataweza kufanya kazi za uandishi wa habari wa
kiuchambuzi kwa kuoanisha habari kutoka vyanzo vya mataifa mbalimbali,
kuandika habari kwa kutumia takwimu kutoka katika mitandao na kutumia
taarifa na hotuba zilizopita zilizotolewa na viongozi wa mataifa
mbalimbali duniani .
Aidha washiriki hao wameonyesha ushirikiano mkubwa katika uchambuzi wa
mada zilizotolewa na wameomba mafunzo kama hayo yatolewe mara nyingi
iwezekanavyo ili kuwakumbusha kuamsha ari ya waandishi.
Mwisho

Saturday, July 13, 2013

RUVUMA WAFANYA MAANDALIZI YA KUMPOKEA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

 Hivi ndivyo mji unavyoonekana leo katika baadhi ya barabara za Manispaa ya Songea
 Gari likisukumwa baada ya kukaa muda mrefu katika garage bubu iliyopo mitaa ya Buhemba
 Mji safi
Hapa ni mtaa wa Dilux magari yakiwa yamepangwa katika utaratibu mzuri
Mji unawake
Wafanya biashara wa matunda katika eneo hili la Dilux wameondolewa kutokana na ujio wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda mkoari Ruvuma
Dereva Yebo wakiwa katika vituo vyao kwa utaratibu mzuri
Gari la Manspaa likiwa kazini maeneo ya bombambili huku wafanya kazi wakiwa wanazoa na njia hii atapita akiwa anaelekea kukagua miradi na kuweka jiwe la msingi katika baadhi ya maeneo
 Hii ni sehemu moja wapo iliyobomolewa vibanda ikiwa ni  kuweka mji safi
Hapa ni maeneo ya Bombambili upakaji wa rangi alama za barabarani ukiendelea siku ya leo kabla ya Waziri mkuu kutua Ruvuma hapo kesho

Habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com

Friday, July 12, 2013

MAGAZETI YA LEO IJUMAAA 12/7/2013 NA YALIYOCHOMOZA


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MAAFISA WAHALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA WATEMBELEA TUJIFUNZE

Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, (Kutoka kushoto) Mweka hazina Bw. Stephen Sindagulu, Mhasibu,  Bw. David Mkande na Mhasibu, Bw Joseph Mazito. na hapo chini pia leo katika ofisi ya Tujifunze Songea



MAAFISA wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, wmetembelea Kituo cha Uchapaji (Rural Press Songea) ambacho ni Kituo cha Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini yenye makao makuu yake Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kwa lengo la kujifunza na kuimarisha uhusiano wa kituo hicho na Halmashauri ya wilaya ya Mbinga.
Kiongozi wa Ziara hiyo fupi ya Maofisa watatu, Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Bw. Stephen Sindagulu, amesema imekuwa ya mafanikio makakubwa kwani wameweza kujionea mahali kazi zao zinapochapwa na kuzungumza na uongozi wake na kuona mitambo iliyopo kiwandani hapo.

Akiwa ameongozana na Wahasibu wawili toka Ofisi yake, Bw. David Mkande na Bw. Joseph Mazito, Mweka Hazina huyo, Bw. Sindagulu, alipata kuziona baadhi ya mashine na kazi zinazofanywa pia kukagua aina mbalimbali ya karatasi kulingana na mahitaji ya wateja kuzihitaji kuchapiwa kazi zao.
 
 Kazi zinazochapwa na Kituo hicho cha Magazeti vijijini Kanda ya Kusini, licha ya kuchapisha Gazeti la Kanda ya Kusini, Tujifunze, huchapa pia   nyaraka mbalimbali za kiserikali za Sekta ya Elimu katika kunyanyua ubora  wa taaluma katika shule za msingi, sekondari na vyuo pia Idara nyingine kama Afya, Kilimo, Utawala na nyinginezo.

Huchapisha pia vitu  mbalimbali  vya watu binafsi na serikali kwa maagizo wayatakayo ikiwa ni pamoja na vitabu vya risiti, tiketi za kusafiria,  stakabadhi za malipo mbalimbali ikiwa ni pampja na fomu za malipo kama TFN 4 na 5.
Mhariri wa Tujifunze, Bw Christian Sikapundwa, ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Mbinga kwa kutembelea Kituo chake na kusema ni mfano wa kuigwa na Halmashauri nyingine katika Kanda ya Kusini.
"Ziara yenu fupi ya kuona kazi zenu huchapwa wapi na kwa ubora gani imepokelewa vizuri, na tunaamini wengine watafuata nyayo zenu,' alisema Bw. Sikapundwa.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inaendeleza uhusiano mwema uliojengeka na Kituo chake toka Enzi ya Mweka hazina wa halmashauri hiyo ambaye sasa amepanda hadi kuwa Katibu Mkuu mmojawapo katika Serikali ya awamu ya Nne , Bw. Rashid Katanga.