Wednesday, July 10, 2013

SHULE YA SEKONDARI LONDON NA MAFANIKIO YAKE


 Mwanafunzi wa Kidato cha III 2013, Japhua Nyumayo, akiwa na Mzazi wake Hindu Said, wakisubiri kumuona Mkuu wa Shule  katika Ofisi Kuu ya Shule ya Sekondari ya Londoni iliyopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma leo.


Mbele ya Jengo la Utawala, Maua yamepandwa kwa mpangilio na kumwagiliwa vyema licha ya msimu huu wa kiangazi  kuwa na jua kali, maua hayo yanaendelea kupendeza na kuifanya shule kuwa ya kijani. Licha ya majengo ya Utawala, Madarasa, Vyoo na Mabweni kutunzwa vema bado ni somo tosha kwa wanajumuia wa shule hiyo na wanaowazunguka kujifunza utunzaji wa usafi na mazingira.


Alama ya Taifa, Bendera ikipepea katika Viwanja vya Shule hiyo ya Kidato cha I-VI ambayo inaendelea kujizolea sifa kitaaluma na nidhamu mkoani Ruvuma na kuwasukuma wazazi na walezi wengi kutaka vijana wao wahamie katika shule hiyo.
Shule hiyo hivi sasa ina Bweni kwaajili ya kulala wasichana. 


Mkuu wa Shule, Mwl. Christopher Mwageni, akiwa Ofisini kwake ambamo huendesha shughuli za utawala na uongozi.  Utawala wake uliojengeka imara kwa ushirikianao wa walimu, wanafunzi na watumishi wengine wa shule kwa msaada wa miongozo ya Bodoi ya Shule, umenyanyua jina la Shule ya Sekondari London  na kuiweka miongoni mwa Shule za  Sekondari za wananchi  bora zinazoiletea sifa serikali mkoani Ruvuma.


Mwalimu wa Shule ya Sekondari London,  Rashid Othman (Kushoto) akizungumza na mzazi wa Mwanafunzi wa shule hiyo .



Wanafunzi wavulana wa Kidato cha IV 2013 wakipata chai wakati wa mapumziko ya saa 4 leo, Jengo linalooonekana pale mbele ni jiko lao. Utaratibu huu wa Chakula shuleni unawawezesha vijana wengi kubaki muda wote shuleni na kuzingatia masomo yao.


Tuesday, July 9, 2013

MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NA WACHORA KATUNI

MAGAZETI YA JUMATANO 10/07/2013 NA YALIYOCHOMOZAA

Magazeti ya Jumatano 10/07/2013, Chadema yajianda kujilinda na yaliyochomoza
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

WEMA NAE, AMTANDIKA MAKOFI MENEJA

 
Wema Sepetu.
Mwaija Salum na Denis Mtima
DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo (jina tunalo) iliyopo Kawe Beach, jijini Dar.

MAELEZO YA MENEJA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.

WEMA, WENZAKE WAZIDIWA NA KILEVI
Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika  saa tano usiku, Wema na marafiki zake  walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.
 
Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.
 
Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?.
WEMA AANZA KAZI YA KUSHUSHA KIPIGO
Aliongeza kuwa swali lake kwa kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani alitoka kwenye gari na kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu kwenye nchi hii.
 
“Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.”
Faili la kesi hiyo linasomeka KW/RB5988/2013, SHAMBULIO. Hadi tunakwenda mitamboni, Wema anasakwa na polisi ili apandishwe mahakamani.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Marehemu Steven Kanumba chenye thamani ya shilingi milioni moja.
 
Hata hivyo, Kanumba aliamua kuifuta kesi hiyo kwa sababu ya kutaka amani. Wakati huo Wema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mjasiriamali aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe.
ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR
Kama vile haitoshi, mwaka 2011, Wema huyohuyo alilikwaa soo jipya, akakamatwa na Polisi wa Oysterbay na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ‘Bob Junior’.
 
Katika kesi hiyo, Hakimu Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema na kumhukumu  kwenda jela miezi sita au faini ya shilingi elfu arobaini ambapo alilipa feha hizo. Wakati huo, Wema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

MAGAZETI YA 09/07/2013 NA YALIYOCHOMOZA

Soma Magazeti ya Tarehe 9/7/2013 Chadema kuukataa mkutano wa amani  na mengine kibao
.
.
.
.
.

Sunday, July 7, 2013

SHEREHE YA MAJAMANDA, NI FURAHA TUPU


Mama mkwe Jafua Bint Abdalah, akicheza na mkamwana wake Hindu Said,  mke wa Bw. Juma Nyumayo,  katika sherehe ya majamanda iliyofanyika nyumbani kwao,  Mshangano Manispaa ya Songea tarehe 7/7/2013. Hapo ni baada ya kupewa zawadi ya khanga na mama mkwe huyo, huku wajukuu waliomsindikiza wakifurahia kwa bibi huyo kulisakata rhumba.


Baadhi ya wageni na wenyeji walioshiriki sherehe hiyo wakishangilia manjonjo ya MC Suzzy.

Thursday, July 4, 2013

LOWASSA ATIKISA MWANZA


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili leo uwanja wa ndege wa Mwanza.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika akisalimiana na Mhe.Lowassa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery Tesha 

Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Lowassa akisalimiana na Shekh Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza uwanjani hapo kumpokea.
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege leo.

Shekh Hassan Kabete wa JASUTA
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee alikuwepo kwenye mapokezi na hapa akisalimiana na Mhe. Lowassa
Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe. Lowassa

Mfanyabiashara maarufu wa Mkoani Arusha na Mjumbe wa NEC (CCM-Taifa) Wilaya ya Arumeru ambaye ni mwekezaji mkubwa wa Jiji la Mwanza naye alikuwepo kumpokea 

Mzee maarufu na Kada wa CCM wa siku nyingi Ally Zagamba akisalimiana na rafiki yake Mhe.Lowassa

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini Kitabu cha wageni VIP baada ya kuwasili leo Jijini Mwanza.

Mwanahabari na Mdau wa Blog hii Peter K. Fabian akisalimiana na Mhe. Lowassa VIP

Umati wa wanawake wa dini ya kisilam waliokuwa wamejipanga nje ya VIP kusalimiana na Mhe.Lowassa

Mama maarufu wa Jijiji Mwanza Mama Magige akiteta jambo na Mhe. Lowassa baada ya kusalimiana naye.

Moja ya wanawake wa kisilam ambaye ni kiongozi akisalimiana  na Mhe. Lowassa 

Wanawake waliojitokeza kumpokea Mhe. Lowassa

Na Peter Fabian
MWANZA.

WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa leo amelitikisa Jiji la Mwanza baada ya mamia ya wananchi,viongozi mbalimbali na wamachinga waendesha pikipiki (Bodaboda) kujitokeza kwa wingi katika mapokezi yaliyoanzia uwanja wa ndege wa Mwanza hadi Mjini kati.

Mapokezi hayo yaliyoongozwa na viongozi wa serikali,madhehebu ya dini,wamachinga ambao ni waendesha pikipiki,wafanyabiashara na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliweza kufunika mapokezi ya awali ya leo asubuhi ya  Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua Kongamano na Mkutano wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba unaofanyika jijini hapa.

Baadhi ya wananchi na wakazi wa Jiji hilo walioongozwa na viongozi wa serikali na Makada mbalimbali wa CCM na Taasisi na Madhehebu ya kidini walifurika kwa mamia kumpokea na wengi wa wananchi walikuwa pembezoni mwa barabara kuu ya kutoka uwanja wandege wakimshangilia huku msafara wake ukiwa na magari zaidi ya 90 na pikipiki zaidi ya 200 zilizopamba msafara huo.

Waziri mkuu mstaafu huyo leo  anataraji kushiriki harambee ya kuchangia kituo cha redio IQRA Fm cha jiji Mwanza ili kusaidia kuongeza usikivu wa matangazo yake na kukidhi haja za kujiendesha katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest kuanzia majira ya saa 1:00 usiku kabla ya tukio hilo Lowassa atatembelea ofisi za Umoja wa Machinga wa jijini Mwanza (SHIUMA) na kisha kuzungumza nao katika ukumbi wa New Mwanza Hotel majira ya saa 4:00 asubuhi.

Mheshimiwa Lowassa katika harambee hiyo anatarajiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge wenzake, makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, wafanyabiashara, Taasisi na makampuni ili kufanikisha adhma na lengo lililokusudiwa kutokana na ushawishi alionao na kwa muonekano wa mapokezi yaliyofanyika uwanja wa ndege imeonyesha Mhe. Lowassa ni kipenzi cha watu na bado ananguvu ya kukubalika kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee ya kituo cha radio IQRA ambayo inaongozwa na taasisi ya kiislamu chini ya BAKWATA mkoa wa Mwanza Shekhe Hassan Kabete alisema maandalizi tayari yamekamilika kwa asilimia 100 yakichagizwa na kuwasili kwa mgeni rasmi Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha.


“Tunayo matumaini kwamba tutatimiza lengo la kile tunachotaraji kukusanya kwenye harambee yetu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400, ambapo tayari mfuko wetu umekwisha kusanya kiasi cha shilingi milioni 190 hivyo tunataraji lengo litafikiwa nap engine kuvukwa” alisema Shekh Kabete.
Via/www.gsengo.blogspot.com