Thursday, June 27, 2013
Wednesday, June 26, 2013
UJIO WA RAIS OBAMA TANZANIA, MAANDALIZI SIO MCHEZO
Na Mwandishi Wetu UJIO wa Rais wa Marekani, Barack Obama ni kufuru tupu, kiasi cha fedha ambacho kinachotumika kugharamia ziara yake peke yake kinazidi mara mbili ya kile kilichoteketea pale mtangulizi wake, George W. Bush, alipotembelea nchini mwaka 2008.
Obama, rais wa kwanza mwenye asili ya Bara la Afrika kutawala Marekani, atawasili nchini Julai Mosi, mwaka huu na kufanya ziara ya siku mbili.
Inaaminika kuwa Bush alipokuja nchini, msafara wake uliigharimu Marekani kiasi cha dola milioni 50 (shilingi bilioni 80) lakini Obama na timu yake watatumia mara mbili ya hapo, yaani dola milioni 100 (shilingi bilioni 160).
Hesabu hiyo, ilimtisha hata Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye aliandika kwa mshangao katika akaunti yake ya Twitter, Jumamosi iliyopita: “Ujio wa Obama Tanzania utaigharimu Marekani dola milioni 100.”
UKUBWA WA MSAFARA
Kwa mujibu wa ziara mbalimbali ambazo Obama alishazifanya tangu alipoingia madarakani Januari 2009, msafara wake huwa na watu zaidi ya 800.

Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani, akiwa na mkewe, Michelle, huongozana na watu 500 ambao ni watumishi wa kawaida wa Ikulu ya Marekani, White House.
Katika wahudumu hao 500, wapo madaktari sita pamoja na wauguzi wengine zaidi ya 30, wapishi na kadhalika.
Msafara wa Obama, haukamiliki bila walinzi karibu 300 ambao jukumu lao huwa ni kumlinda rais huyo kwa ukaribu zaidi.
Kutokana na hesabu hiyo ni wazi kuwa Tanzania itakuwa na msukosuko wa aina yake pale Obama atakapowasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Hata hivyo, kwa vile ndege ya Rais wa Marekani, Air Force One, haina uwezo wa kubeba idadi hiyo ya watu, wengi wao watawasili kwa mafungu wiki hii ili kufanya maandalizi ya ujio wake.
Ulinzi wa Obama.
MASHUSHUSHU KILA KONA
Kuelekea siku ya ujio wa Obama, Jiji la Dar es Salaam, limeshawekwa chini ya ulinzi, mashushushu kutoka Marekani wametanda kila kona kuhakikisha rais huyo hapatwi na zahama yoyote akiwa nchini.
Maofisa wa CIA (Central Intelligence Agency) ambao kiuhalisia ndiyo Idara ya Usalama wa Taifa la Marekani, wanadaiwa kuwepo nchini tangu Januari, mwaka huu, lengo likiwa ni kuratibu na kuhakiki usalama wa nchi.
Vilevile inadaiwa, makomandoo wapatao 400 kutoka Taasisi ya Upelelezi ya Marekani, FBI (Federal Bureau of Investigation), waliwasili nchini kwa mafungu kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, jukumu lao likiwa ni kuweka mambo sawa.
Madai hayo yanajengwa na hoja kwamba hata pale FBI walipojitolea kutoa mchoro wa mtu aliyedaiwa kumpiga risasi na kumuua Padri Evarist Mushi, Machi mwaka huu, ilikuwa ni kwa haraka sana.
“Wale FBI walikuwa hapahapa Tanzania ndiyo maana walijitolea kutoa mchoro wa Padri Mushi kwa haraka sana, ingekuwa wapo Marekani wasigejitolea haraka vile.
“Sema sasa ilikuwa siri kubwa. Taarifa za ujio wa Obama kuja zipo tangu mwaka jana ila zilifanywa siri kwa sababu za kiusalama,” alisema ofisa mmoja wa Ikulu ya Tanzania kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.

ANAKUJA NA MAGARI 21
Kwa mujibu wa taarifa za ziara za Rais Obama, kiongozi huyo husafiri na jumla ya magari 21.
Obama husafiri na gari lake binafsi kama Rais wa Marekani aina Limousine Cadillac, ambalo halilipuki wala kuharibika hata likipigwa na bomu.
Gari hilo likilipuliwa na bomu, matairi peke yake ndiyo huungua lakini hubaki na rimu ambazo hutembea kwa umbali wa kilometa 500 bila wasiwasi.
Limousine Cadillac ambalo ni toleo maalum la mwaka 2009 kwa ajili ya Obama pekee, huambatana na magari mengine 20.
Kutokana na tafsiri hiyo, Obama akiwa nchini, atakuwa na msafara wake uliokamilika na unaojitegemea kwa asilimia 100.
MAGARI 21 YATAKUJA VIPI?
Habari zinasema kuwa Limousine Cadillac ndilo litakalokuja na Air Force One, Julai Mosi, mwaka huu, mengine 20 yatawasili kabla ya ujio wa Obama.
Inaelezwa kuwa sababu ya magari hayo 20 kutokea Marekani ni kwamba utaratibu wa White House unaeleza kuwa msafara wa Rais wa Marekani ndani ya nchi unapaswa kufanana na wowote ule anapokuwa nje ya nchi.
Habari zinaeleza kuwa magari hayo 20, yatawasili na manowari kubwa ya Marekani ambayo inategemea kuwasili nchini wakati wowote kupitia Bahari ya Hindi.
Inaelezwa kuwa kazi nyingine ya manowari hiyo ni kudumisha usalama baharini, kuhakikisha watu wenye lengo la kufanya uvamizi hawafanikiwi kwa njia ya majini katika kipindi hiki cha siku chache kabla ya ujio wa Obama na hata pale akiwepo.
HOTELI ZA NYOTA TANO ZAJAA
Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko umebaini kuwa ujio wa Obama umekuwa na neema kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo karibu zote zimekodiwa jumla.
Hoteli hizo zimechukuliwa na Marekani kwa ajili ya watu watakaombatana na Obama ikiwemo wahudumu pamoja na walinzi mbalimbali.
Inaelezwa, baadhi ya hoteli kuna wateja walihamishwa wiki mbili kabla ili kupisha wageni kutoka Marekani ambao wamekuwa wakiwasili nchini kwa mafungu.
WENYE MAGARI MAPYA WAULA
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wamiliki wa magari mapya yenye nafasi, hususan Toyota Noah, kwao ni neema ya aina yake.
Risasi Mchanganyiko limebaini kuwa wenye magari hayo hutakiwa kuripoti Ubalozi wa Marekani nchini kisha vyombo vyao hupimwa kuona uzima wake.
Habari zinasema, kila mwenye gari ambalo litafuzu vipimo, atalipwa shilingi 200,000 kwa siku katika kipindi chote litakapotumika katika ziara hiyo ya Obama.
BUSH NAYE ANAKUJA
Katika hatua nyingine, Bush ambaye ni Rais wa 43 wa Marekani, atawasili nchini hivi karibuni.
Hii ina maana kuwa kipindi ambacho Obama atakuwepo nchini, Bush naye atakuwepo ndani ya Tanzania.
Bush yeye anakuja kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa wake za marais mbalimbali duniani ambapo imeelezwa kuwa mke wa Obama, Michelle, naye atahudhuria.
KARIBU OBAMA
Ujio wa Obama ni fahari ya Tanzania kwamba nchi yetu ni salama na inavutia ndiyo maana hata kiongozi huyo wa taifa kubwa kabisa duniani, ameweza kushawishika kuja.
Karibu sana Tanzania Rais Obama.

via/boss ngasa blog
Monday, June 24, 2013
POLISI RUVUMA WACHACHAMAA WAKAMATA TENA MENO YA NDOVU YATANGAZA KIAMA KWA MAJANGIRI
Kamanda Nsimeki na Meno ya Ndovu: Patachimbika Ruvuma
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki akipanga meno ya Ndovu kulingana na uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo.
Mwandishi wa habari Amoni Mtega akiwa amenyanyua jino la Ndovu
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya ndovu 18 yenye uzito wa kilo 84 yenye thamani ya Shilingi 216,000,000 sawa na dola 15 elfu za Kimarekani. Kwa meno hayo ni sawa sawa na Tembo tisa waliouwawa kikatili kisa kumiliki meno hayo yanayohitajika na majangiri wasio na huruma na viumbe hivyo vilivyobeba meno yenye thamani kubwa.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, alisema kuwa tukio hilo la kukamata meno hayo lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku katika Kijiji cha Majala Kata ya Nandembo wilayani Tunduru.
Kamanda Nsimeki, alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo lilitokea baada ya askari Polisi wa wilaya hiyo kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa ambao kwa bahati mbaya hawakukamatwa.
Tukio hilo limekuwa la pili la katika kipindi kifupi lile la kwanza lilitokea katika kijiji cha Hanga wilayani Namtumbowsiki mbili zilizopita
Kamanda Nsimeki ametangaza kiama kwa majangiri mkoani Ruvuma na amewataka wajisalimishe la sivyo watakiona cha mtemakuni.
"jeshi la polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao wamejificha na wanajihusha na matukio hayo ya ujangili kwa wanyama na hasa tembo" alisema Nsimeki.
Pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo vya uhalifu wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi na wananchi.
WAFANYAKAZI WA PRESS NCHINI WAKUTANA BAGAMOYO, WAJADILI WELEDI WA UTUMISHI
| Watumishi wakiiimba wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi |
Saturday, June 22, 2013
WATAKAOJIUNGA JKT- MAJINA KIDATO CHA SITA AWAMU YA PILI 2013
MAJINA YA VIJANA KIDATO CHA SITA 2013 MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI NA VIKOSI WALIVYOPANGIWA
Bofya hapo kwenye kambi: au fuata Link hii ya www. jkt.go.tz
Bofya hapo kwenye kambi: au fuata Link hii ya www. jkt.go.tz
Chanzo: Jeshi la Kujenga Taifa
Friday, June 21, 2013
WANAVYOTUSEMA
Katuni via/wavuti
Angalia wanavyotusema, hadi wanatuchora!
Na Juma Nyumayo, Songea
Hapa ni dhahiri hakuna umakini, "what is kubusti Blogu?" ukilinganisha na madhara ya kuua na kufufua?
Hakika kwa mtindo huu, hatutaaminika.
Kwa wote wanaoendesha Blogu na mitandao ya jamii tukianzia na wa mkoani Ruvuma, nchini Tanzania na kwingineko Ulimwenguni, naomba tuwe makini sana kuandika vitu vya ukweli ili kujenga Taswira njema na imani kwa wasomaji wetu.
Blogu na mitandao mingine ya kijamii huwafikia watu wengi kwa haraka hivyo ina umuhim wa kuaminika kila kinachoandikwa.
Blogu ni chombo cha habari lazima kifuate Sheria, Kanuni na taratibu za Chombo cha habari kikiwa na sera zinazoeleweka kwa wasomaji wake. Ni muhimu kuhakikisha Blogu inachapisha na kutangaza vitu vyenye "Ukweli na Kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza."
Publish "The truth and try to minimize harm,". Haitakuwa na maana unachapisha na kutangaza ukweli unaoacha madhara makubwa kwa wasomaji wako na jamii husika. haina maana kabisa.
Mfano unaweka picha zenye muonjo mbaya 'bad taste' wasomaji wako wanaumizwa/ wanakerwa na picha hizo na kuwapa uwezo wa kuamua kutofungua tena Blogu yako.
Hasara hii ni kwa nani katika ulimwengu wa kuhabarishana? Maana yake hasara hii ingeweza kuzuiliwa kwa kufuata misingi ya Chombo cha habari katika maamuzi ya picha gani ichapishwe bila kuomba radhi na ile inayotakiwa ichapishwe kwa kuomba radhi na baadae kuondolewa.
Asante kwa katuni hiyo hapo juu, Inatukumbusha tukiwauwa wote, basi zamu yetu imefika, tujiue na tujifufue. Kumiliki Blogu isiwe sababu ya kuendekeza mabo ya kijinga na kuanza kujenga utamaduni ovyo ovyo.
UNGA WAWAPELEKA JELA MIAKA 15 UGHAIBUNI
Mabondia waliohukumiwa
Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin.
Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.
Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.
Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini.
"Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
"Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea."
"Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000". walisema
Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.
Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka mitano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa kulipa faini ya pauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine Mohabuth in Mauritius, Jaji aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.
Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.
Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.
Chanzo: BBC-Swahili
Subscribe to:
Posts (Atom)