Picha hii ni kwa hisani ya Blog ya VANGONI hapo ndo uvaaji wa wanawake wa kingoni wakiwa wamejipamba kisawasawa. Nimeiona picha hii imenivutia saaana nadhani pia wasomaji wetu watanuafaika na kuvuta hisia miaka hiyo ya 1900.
Wednesday, July 25, 2012
Vimwana wa kingoni
Picha hii ni kwa hisani ya Blog ya VANGONI hapo ndo uvaaji wa wanawake wa kingoni wakiwa wamejipamba kisawasawa. Nimeiona picha hii imenivutia saaana nadhani pia wasomaji wetu watanuafaika na kuvuta hisia miaka hiyo ya 1900.
Salaaaam wote
Wanamtandao nawasalimia woote kabisa. Kwa sasa nipo Dar es Salaam, naendelea kufuatilia story na picha zenu asanteni saana.
Thursday, May 3, 2012
Taasisi ya Elimu Tanzania kujenga stadi za kusoma kuandika na kuhesabu (KKK)
Picha ya kwanza juu: Mkurugenzi wa Chuo kikuu Huria (OUT), Songea Andrew Komba akichangia hoja kuhusu maboresho ya mitaala ya elimu hapa nchini.
WADAU WA ELIMU WAKIPITIA CHANGAMOTO ZA ONGEZEKO LA KUTOJUA KUSOMA KUANDIKA NA KUHESABU
Kikundi cha wadau toka Manispaa na Songea Vijijini wakiibua hoja mbalimbali kuhusu mitaala ya elimu na ongezeko la wasiojua KKK kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hapa mkoani Ruvuma ili zichukuliwe na Taasisis ya elimu Tanzania -TET wazifanyie kazi kuokoa jahazi. ( Picha na Christian Sikapundwa)
Monday, March 26, 2012
Kwanini watu huharibu kumbukumbu?
Barabara Dar kwenda Morogoro eneo la Ubungo linavyoonekana baada ya kupanuliwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.Miaka ya 1995 hadi 2005 Serikali ya awamu ya tatu Waziri Mkuu wakati ule Mheshimiwa Frederick Sumaye chini ya Rais Che Ben Mkapa alifanya maamuzi ambayo hayatasahaulika, kwanza alilivunja Baraza la madiwani wa Jiji la Dar es Salaam akaunda Tume ya Jiji la Dar es Salaa, ikaongozwa na Bw. Keenja Tume ile ilifanya kazi nzuri saana. Pili akaamuru kuvunjwa kwa nyumba zilizopo kandokando ya barabar ya Morogoro tokea pale ubungo kuelekea Kimara kupisha uapanuzi wa barabara hiyo ili Foleni kubwa ya magari ipungue katika hicho kibarabara kimoja na kuwa mbili za kuingia mbili zinatoa. mheshimiwa benjamin Mkapa aliifungua barabara ile mimi nilikuwepo pale Ubungo Minazi karibu na Jengo la Tanesco. Mkapa aliifungua barabara ile pamoja na Kituo kile cha mabasi ya Daladala kwa Mbwembwe kibao akiongozwa na maneno ya uhakika ya kuitunza barabara ile na Dkt. John Pombe Magufuli waziri wake aliyekuwa akiwaita Askari wa mwamvuli pamoja na viongozi wengine kibao wa ndani na nje hasa wale walifadhili ujenzi wa barabara ile. Cha kushangaza leo nimezuru eneo lile na kile kibao kilichoandikwa Tarehe ya ufunguzi kimeng'olewa. Hakuna anayejali. Tabia hii ipo kila mahala sasa. kumbukumbu zapotezwa kwaajili au ya biashara ya chuma chakavu au ni ujinga tu? kwa wale wanaojali historia tabia hii inachukiza sana.
Saturday, March 24, 2012
Kama naanza vile!
Ndugu wapendwa ni kitambo sijawapatia vile vitu mwavitaka. Hii ilitokana na matatizo ya hapa na pale ya ki- technolojia lakini nimekwisha weka mambo sawasawa.
Nimewakosa sana wasomaji wa nje kama kina Yasinta Ngonyani na Prof. Mbele na wenzao huko majuu na wewe msomaji mpendwa hapo ulipo katika anga za hapa nchini, barani Afrika, Asia, Ulaya, Marekani na kwengineko. Naahidi kufanya mabadiliko makubwa tuombeane uzima.

Tuesday, November 15, 2011
TGNP ndani ya Ruvuma kiutafiti zaidi
Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, wapo mkoani Ruvuma kwa utafiti kuelewa ni kwa kiasi gani vyombo vya habari vimecangia katika kutangaza na kusambaza habari kupitia kampenina harakai za Ukombozi wa mwanamke Kimapinduzi katika Mkoa wa Ruvuma.
Utafiti huu unaoumia mbinu za kukusanya taarifa kwa madodoso, majadilianao,kazi za vikundi, maswali ya uchokozi na Uchambuzi wa pamoja inawashirikisha washiriki wa semina zilizowahi kuendeshwa na TGNP mkoani Ruvuma katika Makundi matatu.
Makundi hayo ni Waheshimiwa Madiwani viti Maalum wa Manispaa ya Songea, washiriki toka Asasi zisizo za kiserikali, Vikundi vya wanawake na waandishi wa habari.
Utafiti huu unaoshirikisha zadi yawatu 30 unaongozwa na Bw. Badi Darusi toka TGNP makao Makuu Dar es Salaam, ambapo pichani anamuelekeza Judith Lugoye wa Ruvuma Press Club namna ya kutuma picha katika mitandao mbalimbali.
(Piha na maelezo Juma Nyumayo)

Subscribe to:
Posts (Atom)