Tuesday, July 9, 2013

Sunday, July 7, 2013

SHEREHE YA MAJAMANDA, NI FURAHA TUPU


Mama mkwe Jafua Bint Abdalah, akicheza na mkamwana wake Hindu Said,  mke wa Bw. Juma Nyumayo,  katika sherehe ya majamanda iliyofanyika nyumbani kwao,  Mshangano Manispaa ya Songea tarehe 7/7/2013. Hapo ni baada ya kupewa zawadi ya khanga na mama mkwe huyo, huku wajukuu waliomsindikiza wakifurahia kwa bibi huyo kulisakata rhumba.


Baadhi ya wageni na wenyeji walioshiriki sherehe hiyo wakishangilia manjonjo ya MC Suzzy.

Thursday, July 4, 2013

LOWASSA ATIKISA MWANZA


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili leo uwanja wa ndege wa Mwanza.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika akisalimiana na Mhe.Lowassa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery Tesha 

Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Lowassa akisalimiana na Shekh Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza uwanjani hapo kumpokea.
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege leo.

Shekh Hassan Kabete wa JASUTA
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee alikuwepo kwenye mapokezi na hapa akisalimiana na Mhe. Lowassa
Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe. Lowassa

Mfanyabiashara maarufu wa Mkoani Arusha na Mjumbe wa NEC (CCM-Taifa) Wilaya ya Arumeru ambaye ni mwekezaji mkubwa wa Jiji la Mwanza naye alikuwepo kumpokea 

Mzee maarufu na Kada wa CCM wa siku nyingi Ally Zagamba akisalimiana na rafiki yake Mhe.Lowassa

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini Kitabu cha wageni VIP baada ya kuwasili leo Jijini Mwanza.

Mwanahabari na Mdau wa Blog hii Peter K. Fabian akisalimiana na Mhe. Lowassa VIP

Umati wa wanawake wa dini ya kisilam waliokuwa wamejipanga nje ya VIP kusalimiana na Mhe.Lowassa

Mama maarufu wa Jijiji Mwanza Mama Magige akiteta jambo na Mhe. Lowassa baada ya kusalimiana naye.

Moja ya wanawake wa kisilam ambaye ni kiongozi akisalimiana  na Mhe. Lowassa 

Wanawake waliojitokeza kumpokea Mhe. Lowassa

Na Peter Fabian
MWANZA.

WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa leo amelitikisa Jiji la Mwanza baada ya mamia ya wananchi,viongozi mbalimbali na wamachinga waendesha pikipiki (Bodaboda) kujitokeza kwa wingi katika mapokezi yaliyoanzia uwanja wa ndege wa Mwanza hadi Mjini kati.

Mapokezi hayo yaliyoongozwa na viongozi wa serikali,madhehebu ya dini,wamachinga ambao ni waendesha pikipiki,wafanyabiashara na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliweza kufunika mapokezi ya awali ya leo asubuhi ya  Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua Kongamano na Mkutano wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba unaofanyika jijini hapa.

Baadhi ya wananchi na wakazi wa Jiji hilo walioongozwa na viongozi wa serikali na Makada mbalimbali wa CCM na Taasisi na Madhehebu ya kidini walifurika kwa mamia kumpokea na wengi wa wananchi walikuwa pembezoni mwa barabara kuu ya kutoka uwanja wandege wakimshangilia huku msafara wake ukiwa na magari zaidi ya 90 na pikipiki zaidi ya 200 zilizopamba msafara huo.

Waziri mkuu mstaafu huyo leo  anataraji kushiriki harambee ya kuchangia kituo cha redio IQRA Fm cha jiji Mwanza ili kusaidia kuongeza usikivu wa matangazo yake na kukidhi haja za kujiendesha katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest kuanzia majira ya saa 1:00 usiku kabla ya tukio hilo Lowassa atatembelea ofisi za Umoja wa Machinga wa jijini Mwanza (SHIUMA) na kisha kuzungumza nao katika ukumbi wa New Mwanza Hotel majira ya saa 4:00 asubuhi.

Mheshimiwa Lowassa katika harambee hiyo anatarajiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge wenzake, makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, wafanyabiashara, Taasisi na makampuni ili kufanikisha adhma na lengo lililokusudiwa kutokana na ushawishi alionao na kwa muonekano wa mapokezi yaliyofanyika uwanja wa ndege imeonyesha Mhe. Lowassa ni kipenzi cha watu na bado ananguvu ya kukubalika kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee ya kituo cha radio IQRA ambayo inaongozwa na taasisi ya kiislamu chini ya BAKWATA mkoa wa Mwanza Shekhe Hassan Kabete alisema maandalizi tayari yamekamilika kwa asilimia 100 yakichagizwa na kuwasili kwa mgeni rasmi Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha.


“Tunayo matumaini kwamba tutatimiza lengo la kile tunachotaraji kukusanya kwenye harambee yetu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400, ambapo tayari mfuko wetu umekwisha kusanya kiasi cha shilingi milioni 190 hivyo tunataraji lengo litafikiwa nap engine kuvukwa” alisema Shekh Kabete.
Via/www.gsengo.blogspot.com

BANGO LA SHIRIKA

Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali Mkoa wa Ruvuma (RUNECISO) Bw. Adam Nindi akikiangalia kibao kinachoonesha ofisi yake ilipo Manispaa ya Songea  juzi. Uwepo wa vibao kama hivi kwa Ofisi za serikali, Mashirika na Shule za Msingi na sekondari ni muhimu sana kwa wadau kuokoa muda wa kuzifikia na kuhudumiwa.

TAKUKURU RUVUMA YACHOMOA MAKUCHA YAKE, YAWAPANDISHA KIZIMBANI WATUMISHI WA UMMA 12

 Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Ruvuma Juu ya Kuwafikisha mahakamani watumishi 12 wa halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kujibu mashtaka mbalimbali ya rushwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002 .


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA


Mkuu wa Takukuru Ruvuma, Daudi Masiko

S. L. P. 926,
SONGEA – RUVUMA, TANZANIA.

Anwani ya simu: “UCHUNGUZI”
Simu Nambari: 025 2600613
Nambari ya Nukushi: 025 2600663
Barua pepe:
rbcruvuma@pccb.go.tz
Simu ya Bure: 113 
--
Katika siku za hivi karibuni, TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imewafikisha mahakamani watumishi 12 wa halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kujibu mashtaka mbalimbali ya rushwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002 . Washitakiwa waliofikishwa mahakamani ni kama ifuatavyo:

  • ECONOMIC CASE No. 1/2013 – Katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga
WASHTAKIWA:

         1. ANTONY SIMON MASHIMBA (65) – EX District Medical Officer
        
 2. FRANCIS FAUSTUS (56) – Coordinator  HIV/AIDS Project - Mbinga
       
  3. JOHN MANDALA (51) – Assistant Accountant – Mbinga District

 
MASHTAKA:

Watuhumiwa walifikishwa mahakamani tarehe 24/04/2013 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 1/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga. Wameshtakiwa kwa 
 makosa mawili kinyume na kifungu cha 28(1) cha PCCA Na. 11/2007 na kifungu cha 
57(1)  na 60(2) cha sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002.
  • ECONOMIC CASE No. 2/2013 – Katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga
WASHTAKIWA:

                        1. PASCHAL J. MAKOYE (36) – Mweka Hazina (W) Mbinga
                       
 2. ROBERT K. MARANDA (42) – Boharia (W) – Mbinga

 
MASHTAKA:
Watuhumiwa walifikishwa mahakamani tarehe 03/05/2013 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 2/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Mbinga. Wameshtakiwa kwa makosa sita kinyume na vifungu vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002.
  • ECONOMIC CASE No. 2/2013 – Katika mahakama ya Wilaya ya Namtumbo
MSHTAKIWA:

                        BRUNO N. MFIKWA (47) – EX-Clinical officer, Namtumbo District

MASHTAKA:

Shauri hili lilifikishwa mahakamani tarehe 03/05/2013 na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 2/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Namtumbo. Mshitakiwa anakabiliwa na makosa nne kinyume na vifungu vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007, sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002 na sheria ya uhujumu uchumi Cap. 200 R.E 2002.
  • CRIMINAL CASE No. 54/2013  – Katika mahakama ya Wilaya ya Tunduru
MSHTAKIWA:

YUSUF SELEMANI MATUMLA (31) – VEO, Kijiji cha Majala –Tunduru

MASHTAKA:

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani tarehe 29/05/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 54/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Tundurukwa kutenda makosa tisa (9) ya rushwa kinyume na K/F 15 cha PCCA Na. 11/2007.
  • CRIMINAL CASE No. 54/2013  – Katika mahakama ya Wilaya ya Tunduru
MSHTAKIWA:

                     FITINA ADAM MBUYU (38) – VEO, Kijiji cha Tuleane - Tunduru

MASHTAKA:

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani tarehe 14/06/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 60/2013 katika mahakama ya Wilaya ya Tundurukwa kutenda kosa la rushwa kinyume na K/F 15 cha PCCA Na. 11/2007.
  • CRIMINAL CASE No. 93/2013  – Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea
MSHTAKIWA:
               
   ERNEST IRENEUS HAULE (33) – VEO, Kijiji cha Liganga - Songea

 
MASHTAKA:

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani tarehe 25/06/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 93/2013 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea kwa kutenda makosa mawili ya rushwa kinyume na vifungu vya 28(1) na 31 vya PCCA Na. 11/2007.

  • CRIMINAL CASE No. 92/2013 – Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea 
  •  
  • WASHTAKIWA:

         1. BARNABAS B. MTWEVE (54) – HIV/AIDS Coordinator  Songea
       
  2. STEPHEN ANDREW MHANDO (61) – Ex- Ag. DMO Songea
        
 3. MICHAEL JOSEPH SIAJABU (46) – Katibu wa Afya Wilaya Songea
       
  4. CLEMENTINA BEDDDA NGONYANI (71) – Meneja wa ukumbi wa EMAU Peramiho.


MASHTAKA:

Watuhumiwa walifikishwa mahakamani tarehe 25/06/2013 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 92/2013 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Songea. Wameshtakiwa kwa makosa kumi na tano (15) kinyume na vifungu vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007 na sheria ya kanuni ya adhabu Cap. 16 R.E 2002.


IMETOLEWA NA DAUDI MASIKO
MKUU WA TAKUKURU (M) RUVUMA

JESHI LA MISRI LAMWANGUSHA RAIS MURSI KWA KUKAIDI USHAURI ALIOPEWA


 HATMA YA AFRIKA: MAPINDUZI NA UJENZI WA DEMOKRASIA  KATIKA MATAIFA YA KIARABU. Egypt's Chief of Staff General Abdulfettah es Sisi announced the president of the constitutional court to task presidency until the elections. (video captured) (Anadolu Agency - Egyptian TV) 
Keine Weitergabe an Drittverwerter.
MAELFU ya Wamisri wanasherehekea kupinduliwa Rais Mohammed Mursi, huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi limeanza kuwakamata viongozi wa juu wa Udugu wa Kiislamu na wasiwasi ikiwa hatua hii italeta muafaka wa kisiasa. 

Kwa siku nzima ya jana (03 Julai), watu walikuwa wakisubiri kwa hamu muda wa mwisho aliopewa Rais Mursi na jeshi, na jioni yake maelfu ya wapinzani wa kiongozi huyo wa mwanzo kuchaguliwa kidemokrasia walizidi kumiminika kwenye viwanja vya Tahrir na kasri ya rais. 

Hali ilikuwa ya amani zaidi kuliko ilivyokuwa katika siku za hivi karibuni.

Pale waziri wa ulinzi alipoanza kutoa hotuba yake iliyongojewa kwa hamu na kwa muda mrefu, umma ulip
iga kelele za “Amani!Amani!”, lakini dakika chache baadaye umma huo ukaripuka kwa vifijo na nderemo na uwanja wa Tahriri ukageuka mara moja kuwa uwanja wa tamasha. 

Fashifashi zikalitanda anga, na watu wakavaana miilini huku wakifuta machozi ya furaha. Sharif, profesa wa chuo kikuu ni mmoja wao.

“Nina furaha ya kunichania nguo hapa, kuona kwamba Wamisri wa kila tabaka wapo uwanjani. 

Mtu anaweza kusema kwamba huku ni kuachiliwa uhuru wetu kutoka gerezani mwa wenye siasa kali. Udugu wa Kiislamu wamesababisha matatizo mengi sana.” Amesema Sharif.

Sharif alisisitiza kwamba wote ni Wamisri na sio Waislamu au Wakristo, kwamba kwa miaka 7000 wamekuwa wakinywa maji mamoja na wakivuta hewa moja. Kando ya Sharif, mtu mwengine alijiangusha chini na kusujudu kumshukuru Mungu, huku macho yake yamerowa machozi.

Bado kungali na maswali kadhaa
Maafisa wa jeshi wakishangiria baada ya Mursi kutangazwa amepinduliwa. Maafisa wa jeshi wakishangiria baada ya Mursi kutangazwa amepinduliwa.
 
Lakini kando ya furaha hizi kubwa, watu hawa waliopeperusha bendera kulipongeza jeshi kwa kumuondoa Mursi, bado wana maswali kadhaa ya kujijibu. Jeshi, upinzani, wawakilishi wa Kanisa la Koptik na wa dini ya Kiislamu, walisema wamekubaliana kwamba Mkuu wa Mahakama ya Kikatiba awe rais wa kipindi cha mpito, lakini utaratibu mzima kuelekea uchaguzi mpya bado hauko wazi.

Pia haifahamiki hatima ya Rais Mursi na wenzake wa kundi la Udugu wa Kiislamu, ambao taarifa zinasema wanashikiliwa na jeshi. Baadhi ya walio Uwanja wa Tahriri, kama Nadir, wanapajua wanapotaka Mursi awepo kwa sasa.

“Lazima awe yuko gerezani na lazima mumshitaki. Watu wengi wameuawa wakati wa uongozi wake na hatuwezi kuwasahau.” Anasema Nadir.

Lakini Mursi alikuwa rais wa kwanza kuingia madarakani kupitia uchaguzi wa kidemokrasia, akishinda zaidi ya asilimia 50 ya kura, na hivyo uhalali na nguvu zake haziwezi kupuuziwa kisiasa na hata kisheria.

Bado haifahamiki ikiwa wafuasi wa Udugu wa Kiislamu, ambao waliripuka kwa ghadhabu wakati mkuu wa majeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Sisi, alipokuwa akitangaza mapinduzi yake usiku wa jana, watajiunga na kipindi cha mpito, ama nao wataendelea kuandamana na hivyo kuikwamisha tena nchi kisiasa.

Kwa vyovyote vile, bado mambo hayajesha kwenye taifa hilo kongwe kaskazini mwa Afrika.
via/jumamtanda blog

Monday, July 1, 2013