Friday, November 16, 2012

Shirika la Kuhudumia wazee PADI lapata Tuzo

Na Juma Nyumayo, Dar

KATIKA hali ya kutia moyo na kuridhishwa kiutendaji, Shirika la Tanzania Mission To tha Poor and Disabled (PADI) lenye makao yake makuu, Mjini Songea mkoa wa Ruvuma limepata Tuzo likiwa ni Mshindi wa kwanza katika kuwahudumia watu hasa wazee na kusukuma mambo ya kisera serikalini.
Kabla ya ugawaji wa Tuzo hizo maelezo yalitolewa na viongozi wa The Foundation for Civil Society, na akaombwa Mgeni rasmi wa hafla hiyo kutoa Tuzo hiyo.
Tuzo hiyo si zwadi kwa Mtendaji Mkuu wa PADI Bw. Iskaka Msigwa na watumishi wenzake bali kwa Mashirika yote ya Mkoa wa Ruvuma, Serikali, wazee wenyewe na watu wote wa Songea ambao wamethibitishiwa kuwa kazi za PADI zimekubalika hapa nchini
Hongera PADI,

Tamasha la 10 Asasi za kiraia Tanzania 2012 lamalizika

Na Juma Nyumayo, Blue Pearl, Ubungo Plaza--Dar Es Salaam,

Tamasha la siku tatu la asasi za kiraia nchini lililoandaliwa na The Foundation for Civil Society limemalizika jioni hii kwa mafanikio makubwa.
tamasha la Mwaka huu lilikuwa na kauli mbiu ya wajibu wa asasi za kiraia katika mchakato wa kuandika katiba mpya nchini.
Asasi zaidi ya 10 ziliwakilishwa hapa kupitia Mitandao ya wilaya, Mikoa au mashirika miamvuli ambapo washiriki zaidi ya 420 walihudhuria toka mikoa yote ya zamani na iliyoundwa (mipya) toka bara na Visiwani.
Maswala kadhaa yamejadiliwa mengine yakipatiwa ufumbuzi mengine yakizua mijadala ya kitaifa lakini kubwa ni kulenga kupata katiba nzuri itakayotokana na mawazo na mahitaji halisi ya watanzania wenyewe.
Sintofahamu iliwakuimba wajumbe baada ya wasomi waliobobea katika nyanja za kisheria walipogusa kuwa KATIBA wanayoitaka ni ya nchi gani? kwakuiwa mpaka sasa Muungano wetu una nyufa kadhaa, wakati ambapo Wazanzibari wana Katiba yao, nchi yao na watu wa bara hawana Tanganyika  yao> Hivyo suala la Muungano limetakiwa kujadiliwa na kupatiwa muafaka.

Tuesday, October 2, 2012

Bodi mpya ya UTPC yazinduliwa Mwanza

Bodi Mpya ya Muunganowa Club za waandishi wa habari nchini, UTPC imezinduliwa Jijini Mwanza baada ya kuagwa ya zamani.
Bodi hiyo itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu ijayo.
Bodi mya inatazamiwa kuendeleza kuvijengea uwezo vyama vya waandishi wa habari mikoani katika mafunzo na weledi wa kazi hiyobila kusahau maadili.
Bodi ya zamani ilikuwa na wajumbe wafuatao.
Ken Simbaya --rais
Zilipa Josph  makamu wa rais
Juma Nyumayo
Mary Edward
Ali Haji hamadi
Hassan hashim
Devotha Minja
Jimmy Luhende
Deo Nsokolo
Lucy Ogutu

Kati ya hao watatu wanaendele nao Ni Ken Simbaya, Ali haji hamadi na Deo Nsokolo

Friday, September 21, 2012

Wazazi wawajibike kuwatunza wanafunzi waliomaliza Mitihani yao jana

Wazazi na walezi wa wanafunzi waliomaliza mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi hapa nchini jana (20/09/2012 wameombwa kuwalea kwa karibu watoto hao kimaadili wakiwa wanasubiri matokeo ya Mtihani huo muhimu.
Hayo yamesemwa na wanataaluma mbalimbali waliozungumza na mtandao huu wa www.ruvumapress.blogspot.com mjini Songea.
Wamesema licha ya wadau wa elimu kulaumu mtindo uliotumika wa kujibu maswali hata yale ya Hisabati kwa mtindo wa kuchagua, bado Elimu ya watoto hao ipo mikononi mwa wazazi na walezi.
Swala la Elimu bora au bora elimu sasa halina nafasi na kwamba ni muhimu kuitafuta elimu kwa kila namna.
Wanafunzi wengi  wanapomaliza mitihani yao huonekana wamemaliza elimu na kujikita kwenye shughuli ambazo hata umri wao haulingani.

Saturday, September 15, 2012

WIZARA YA ELIMU YATANGAZA MTIHANI KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2012



Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Mtihani Wa Kumaliza Elimu Ya Msingi Mwaka 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2012

JAMHURI2 YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI



Ndugu wananchi,
Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Tanzania Bara utafanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012. Jumla ya wanafunzi 894,881 wamesajiliwa kufanya mtihani huo ambapo wavulana ni 426,285 sawa na asilimia 47.64 na wasichana ni 468,596 sawa na asilimia 52.36.

Aidha, kati ya wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379 watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 watafanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.

Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39. Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.Mtihani huu utafanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia teknolojia mpya ya ‘Optical Mark Reader’ (OMR), ambapo watahiniwa watatumia fomu maalum za OMR kujibia mtihani na majibu yao yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta.

Masomo yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, English Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.

Ndugu wananchi,Maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani, kusambazwa kwa fomu maalum za kujibia mtihani na nyaraka zote zinazohusu mtihani huo. Mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi ya fomu za OMR yamefanyika kwa lengo la kuwaandaa watahiniwa, wasimamizi pamoja na viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali ili waweze kutumia ipasavyo teknolojia hiyo.

Ndugu wananchi,Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa kuwa unahitimisha ngazi ya Elimu ya Msingi na kufungua milango kwa ajili ya elimu ya sekondari.

Hivyo, matokeo ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na Elimu ya Sekondari.

Kwa kuzingatia umuhimu wa mtihani huo, napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa salama na tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.Napenda pia kutoa wito kwa wasimamizi wa mitihani kufanya kazi yao ya kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu. Wapo baadhi ya wasimamizi ambao wamekuwa wakishiriki katika kuwasaidia watahiniwa kufanya udanganyifu kwenye mitihani.

Napenda kuwaasa tena wasimamizi kujiepusha na vitendo hivyo vya udanganyifu kwani serikali haitasita kuchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani.

Kwa upande wa wanafunzi watakaofanya mtihani mwaka huu, ninaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha miaka saba ya Elimu ya Msingi. Hivyo, ni matarajio yangu kuwa mtaufanya mtihani huo kwa utulivu na kuzingatia taratibu zote za mitihani ili matokeo ya mtihani yaoneshe uwezo wenu halisi kulingana na maarifa na ujuzi mliopata katika Elimu ya Msingi. Serikali inawaasa wanafunzi wote kutojihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu katika mtihani kwani watakaobainika watafutiwa matokeo yao yote ya mtihani. Ndugu wananchi,

Natoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa katika kuhakikisha kwamba mtihani huo unafanyika kwa amani na utulivu wa kutosha bila usumbufu unaoweza kusababishwa na shughuli za kijamii hasa katika maeneo ya jirani na shule.

Mwisho, napenda kuwaasa tena wanafunzi, walimu na wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yoyote katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi.

Nawaomba pia raia wema wasisite kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapoona au kuhisi mtu au kikundi cha watu kinajihusisha na udanganyifu wa aina yoyote katika mtihani huo.Nawatakia watahiniwa wote heri na fanaka katika mtihani utakaofanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.

MHESHIMIWA PHILIPO AUGUSTINO MULUGO (MB) NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI15 SEPTEMBA, 2012

Jua Kali hadi mifukoni hapa Songea



Hakika hali ya uchumi hapa Songea waweza kuiona sehemu za masoko na hasa katika vitoweo.


"...jua kali hadi mifukoni." Wengi wanalia.

Hapa nilikuwa napita mitaa mbalimbali nikatokea eneo la Soko kuu la Songea pale wanawake wanapouza samaki wa kutoka Ziwa Nyasa ambalo linamzozo wa Mpaka Kati ya Tanzania na Malawi,

Samaki aina ya Mbasa, Mbufu, Mbelele na dagaa wale wadogo wa dogo na wakubwa ni maarufu sana, wanauzwa chini tu bila kujali, (Picha inajieleza)

Watamu, wanapendwa.

Nilisimamisha Gari eneo la Magharibi ya Soko Kuu la Songea amabako kuna mlango mdogo wa kutokea maarufu kwa kuuza samaki na dagaa kwa muda wa nusu saa sikuona mteja kuulizia samaki hao, Mama aliyekuwa akiuza kajifunika tu na Mwamvuli.

Mifuko ya wanunuzi nayo imepigwa na jua.

Haina miamvuli .