Saturday, September 15, 2012

DMI wafanya maandamano kuadhimisha siku yao Songea

Shirika la Masista wa DMI, limefanya maandamano makubwa na maonyesho ya Bidhaa mbalmbali mkoani Ruvuma kuadhimisha siku yao hapa nchini.
Masista hao wa madhehebu ya Katoliki wanaojishughulisha na maendeleo ya wanawake, watoto na watu wenye mahitaji maalum katika nchi kadhaa barani Asia, Afrika na kwengineko,walifanya maandamano hayo katika mitaaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupita katika Barabara ya Sokoine eneo la Soko la Songea mjini, Ukumbi wa Manispaa Songea na kuishia Viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ambako mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu, aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti, aliyapokea maandamano hayo, kukagua maonesho na kuwahutubia. Jambo jema ni mabango yaliyobebwa na waandamanaji yaliyodai wtoto yatima kupewa elimu, chakula na kusikilizwa. (Picha zote, Maelezo na Juma Nyumayo)


























ZM Mwanamuziki anayetamba Ruvuma arejea toka Dar



Kijana machachari katika kuimba, Zuberi Mohamedi, Maarufu kama ZM, Mwanamuziki wa kizazi kipya anayetamba kwa vibao vikali mkoani Ruvuma (Pichani Kulia ) akiwa na rafiki yake S. Komba ,wakitokea Kituo cha Redio Jogoo mjini Songea kuwafahamisha wapenzi wao kuwa amerejea toka Dar alikokwenda kujifua na kujinoa hadi kuachia Single moja akiwa na nguli wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature.

Hapo akiwa mitaa ya Soko kuu Mjini Songea karibu na NBC Bank Jengo hilo Jeupe kushoto, alipokutana nami akifanya mipango ya kwenda Madaba kusuuza nyoyo za wapenzi wake baada ya kupotea kitambo.

ZM alinishukuru kwakuwa nilimsaidia kumrusha katika Kituo cha TV Tunduru kwa mara ya kwanza na watu kumuona kwenye runinga tangu azaliwe. hayo yalifanyika wakati alipoanza muziki huo miaka ya 2000 mwanzoni. (Picha na Juma Nyumayo)

Wednesday, September 12, 2012

Ni haki Watoto wa Wakulima na wafanyakazi kuua?




PICHA NO Na 2:Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma, (Kuanzia kushoto) Nathan Mtega wa Radio One, Amon Mtega wa Jamboleo, Joseph Mwambije wa Majira na Muhidin Amri wa HabariLeo wakiangalia Picha ya mabaki ya aliyekuwa Mwandishi wa habari wa ChannelTen, Daud Mwangosi aliyeuawa kwa bomu huko Nyololo Iringa. Tukio hili walilifanya Tarehe 11, Septemba 2012, kabla ya Maandamano ya waandishi mkoani hapa kugonga Mwamba kutokana na sintofahamu ya Viongozi wa Ruvuma Press Club na wasaidizi wao kukosa mawasiliano na Waaandishi wenzao.


PICHA ya Kwanza: Baadhi ya wandishi wakiwa nje ya Ofisi ya Mwakilishi wa Radio One mkoani Ruvuma wakisubiri Maelekezo ya Maandamano ambayo hayakufanyika.


Picha ya Tatu: Askari waliomsulubu Mwangois hadi kumuua kwa Bomu na Kumjeruhi Mkubwa wao ambaye amenyosha fimbo juu.




Wote hao juu ni watoto wa wakulima na wafanyakazi wa nchi hii hakuna mwenyehaki ya kumuua mwenzie hasa wawapo kazini wakitafuta ridhiki kwa njia halali.




























Mtuhumiwa afikishwa Mahakamani, Mkono wa Sheria, haujali Bomu.

Vilio, Simanzi, Maandamano ya wanahabari na wadau wao huenda yakapozwa na hatua ya Mtu anayetuhumiwa kumuua Daud Mwangosi aliyekuwa mwandishi wa Habari wa ChannelTen na Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari mkoa wa Iringa, Tarehe 2, Septemba 2012 kufikishwa mahakamani.

Si Mwingine ni huyo hapo aliyejifunika kichwa chake. Aibu. Ni Aibu kwake.
Bado Jamii ya watanzania wanataka wale waliomtuma kufanya hivyo kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mkono wa Sheria haujali Bomu.
Unajali ukweli ili utende haki.
(Picha kwa Hisani ya Blogu ya www.francisgodwin.blogspot.com









Tuesday, September 11, 2012

Maandamano waandishi yagonga mwamba Ruvuma



Na Gideon Mwakanosya na Nathan Mtega ,Songea

MGOGORO mkubwa umeibika kwa waandishi wa habari mkoani Ruvuma baada ya Viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoani humo kutoitisha maandamano na kuingia mafichoni kwa muda ili kuepusha kufanyika maandamano ya kuunga mkono maombolezo ya kifo cha mwandishi wa habari na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi aliyefariki kwa kupigwa na mlipuko uliosababishwa na polisi katika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa.

Mgogoro huo umewagawa waandishi wa habari na kuwafanya baadhi ya waandishi kutishia kujitoa nafasi zao za uongozi na uanachama.

Waandishi wa habari mkoani Ruvuma walianza kwa walishangazwa na hatua ya viongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho kutowajulisha muda na njia zitakazotumika kwa maandamano hayo hadi pale kwa njia ya simu na baadhi ya waandishi wa habari ambao walishapanga waandamane saa 10. Jioni baada ya kujihakikishia kuwa viongozi wao wamewatosa nan hawana ajenda muhimu ya kupinga m,aandamano hayo kwa hula.

Awali baadhi ya waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali ambao ni wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoani humo (RPC) walijikusanya pamoja na kufuatilia matangazo ya vyombo mbali mbali vya habari yaliyokuwa yakiendelea huku wakiangalia baadhi ya picha zilizopigwa wakati na baada ya kifo cha mwandishi huyo wa habari ambaye alipatwa na mauti wakati akiwa kazini na walipanga wandamane saa 10 jioni muda ambao ndio Marehemu Mwangosi aliuuawa kinyama kupigwa na bomu na Polisi.

Katibu Msaidizi was Chama cha wqaandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma , Julius Konala, alionyesha ushirikiano mkubwa kwa wanachama ambao muda wote walikuwa wanadai rauba na hatua iliyofikiwa na viongozi wa chama hicho kwaqajili yua maandamano na kuwajulisha kuwa viongozi wake hawajulikani waliko na wanapinga kufanyika kwa mnaandamano hayo.

“Jamani mimi mtanionea tuu, Mwenyekiti na katubu wamesema kuwa UTPC imeyasimamisha maandamano yetu bila kutaja sababu,” alisema Konala ambaye alichukua hatua ya kuwasiliana na viongozi wa polisi mkoani hapa waliotaka kujua ni njia zipi zitakazotumiak katiak maandamano hayo ili walete askari waq kuyalinda maandamano hayo ya amani.

Tukio hilo limewakasirisha sana viongozi wa Chama hicho na kulazimika kuitisha mkutano wa dharura kwa baadshi ya wanachjama wengi wao wakiwa ni mamluki na kusababisha viongozi hao kuomba radhi kwamba wamekosa mawasiliano nao na baadhi ya wanachama wametushia kujiuzulu akuwemo katibu msaidizi Julius Konala kwa madai kwamba chama hicho kimeingiliwa na mikono ya wanasiasa.
“naona mbele yangu kuna wingu kubwa ambalo mwisho wake siujui, nafikiria kujiuzulu uongozi na kujitoa kataika chama, “ alisema Konala.

Baadhi ya wadau wa habari mkoani humo wamenesha kushangazwa na ukimya wa wanahabari wa mkoa huo liocha ya wanahabari wote nchini wakionekasna kwenye runinga wakiandamana kupinga ukatili huo iliofanywa dhidi ya Mwandishi wa habari akiwa kazini.

Hata hivyo Mkurugenzi wa muungano wa Vyama vya waandishi wa habari nchini UTPC Abubakar Karsan akiongea na Nipashe kwa njia ya Simu amekanusha vikali kwamba wao walitoa maelekezo kwa Ruvuma Press Club kwamba wasiandamane kwa madai kuwa viongozi hao waliwajulisha kuwa maandamano hayo yatatekwa na CHADEMA.
Mwisho

Monday, September 10, 2012

Nitakulilia daima, ukatili huuhukufanyiwa wewe tumefanyiwa sisi



Samahani kwa kuweka Masalia ya Mwili wa Daud Mwangosi, Mwandishi wa habari wa Channel Ten aliyeuawa kikaqtili baada ya kulipuliwa na Bomu mikonon mwa Polisi. Tutamlilia, machozi yetu yamwgilie mbegu za upendo kwa Polisi wa Tanzania pamoja na viongozi wanaowatuma kutekeleza unyama kwa raia wanaotakiwa kuwalinda.Mwangosi tunakulilia wenzio, najua hutusijii, wakatili wako wanatusikia wanatuona na kesho watatuona tukiandamana. Si kwaajili yako ni kwaajili yetu, watoto wetu na wao pia

Starehe kwa Amani Mwangosi, Msiba wako ni maumivu makubwa na mateso makubwa kwa taifa hili.

Mandamano ya Waandishi Ruvuma

Habari za kuandamana kwa waandishi wa Habari nchi nzima zimepokelewa na wadau wa habari kwa hisia tofauti mkoani Ruvuma.
Wadau kadhaa waliozungumza na Blogu hii wameunga mkono hatua za waandishi kujitetea dhidi ya nguvu kubwa, ukatili, uonevu na dharau ya kazi za wanahabari wawapo kazini hasa pale wanapowapiga, kunyng'anya vifaa vyao vya kazi na vunjajungu pale alipouawa kinyama Mwandishi wa TV ChannelTen Mkoani Iringa Bwana Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Club ya Waandishi mkoni humo (IPC) kwa kulipuliwa na Bomu akiwa mikononi mwa Polisi ambao walikuwa na wajibu wa Kulinda uhai wake.



PICHA: Waandishi wa Habari wakiwa Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu wakipat hbari za maendeleo ya mkoa huo ili kuhabarisha umma hivi Karibuni


PICHA WALIOPO NA GARI NA MITAMBO: Waandishi wa TBC1 wakiunganisha matangazo ya nje wakati wa Sherehe za Eid El Fitr mara baada ya Kumaliza Mfungo wa mwezi wa Ramadhani Agosti, 2012. Je ni uungwana waandishi hawa kuwatesa, kuwadharau kuwanyanyasa na hata kuwauwa kwa kuwalipua na mabomu kama walivyofanya polisi kumuua kikatili Daud Mwangosi wa Iringa????????PICHA