Pages

Thursday, May 30, 2013

KADA MAARUFU WA CCM SONGEA, BW. MATHIAS NYONI , APATWA NA MSIBA WA MKEWE, WENGI WAQHUDHURIA MAZISHI


Kada wa CCM Wilaya ya Songea Mjini na Fundi Cherehani Maarufu, Bw. Mathias Nyoni (wa kwanza kulia) mara baada ya kumaliza kumhifadhi mkewe Salama aliyefariki jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Namanditi kwa  kaleza nje kidogo ya mji njia ya  kuelekea Peramiho


Dua za mwisho kwa Mke wa Bw. Mathias Nyoni, hiyo ndio nyumba yake katika pumziko lake la milele.


Sheikh Abdalah Ndege aliyevaa kofia akitoa maelekezo ya watu mashuhuri waliofika katika msiba huo na kuwaomba watoe neon akiwepo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea mjini, Bw. Mhenga.



Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini, Bw. Mhenga akiwashukuru wananchi na kutoa rambirambi zake kwaniaba ya wana CCM Songea Mjini leo katika Makaburi ya Namanditi. Bw. Mhenga amewashukuru watu wote wakiwemo wa vyama vya upinzani, wafanyabiashara, wakulima na kutoka makundi ya vijana wanawake na wazee kwa kujitokeza kwa wingi kumzika mke wa Kada wa CCM  Salama na kwamba huo ndio msimamo wa CCM katika kuijenga nchi kuwa na amani.


Watu walioshirioki mazishi wakisikiliza shukurani toka kwa familia ya marehemu toka kwa Sheikh Abdala Ndege, aliyesimama kati ya wazee wawili waliokaa


Mhe. Meya wa Manispaa ya Songea, Charles Mhagama,( wa kwanza kushoto)  akiongoza watu toka makaburini eneo la Namanditi Manispaa ya Songea mara baada ya kuzika Alasiri ya leo


Watu wanaendelea kutawanyika toka makaburini


Kila mmoja natafuta usafiri wake kurejea alikotoka wengi wao wakitokea katikati ya mji wa Songea leo


Kina mama nao walikuwepo kwa wingi kumsindikiza Mke wa Mathias Nyoni, Salama ambaye pia alikuwa ni  Mtaalamu wa kuendesha Saloon mjini Songea


Baadhi ya vyombo vya usafiri vilivyowaleta watu ukiachilia mbali daladala zilizoleta watu kwa wingi katika msiba huo ambao ulikusanya watu wa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi, watumishi wa serikali, wafanyabiashara, wakulima na wanachama wa vyama mbalimbali wakiongozwa na wana CCM wa wilaya ya Songea Mjini. (Picha zote na Maelezo na Juma Nyumayo)


ZULU KUZIKWA SONGEA BAADA YA MWILI WAKE KUREJESHWA TOKA MALAYSIA

 MWILI WA ERNEST ZULU WAREJESHWA NYUMBANI

The late Ernest Zulu
Bw. Ernest Zulu

 

Waombolezaji wakitoa mwili wa marehemu Zulu kuiingiza kwenye gari

MWILI wa Ofisa Habari Mkuu wa Bunge, Ernest Zulu (56) aliyefariki Mei 23 mwaka huu nchini Malaysia alikokuwa masomoni, umewasili nchini majira ya saa 1.30 asubuhi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar.
Majira ya mchana mke wake Theresia Zulu na watoto wake walifika kumtambua marehemu na kisha kundi la waombolezaji lilimsindikiza marehemu katika gari  ili kuanza safari yake ya mwisho kabla ya kwenda kupu
mzika milele kijiji kwao ndilima, Songea vijijini.
Kwa wakazi wa dare s salaam Zulu ataagwa kesho nyumbani kwake Ubungo Kibangu.
Baadhi ya watu waliokuwapo mchana wa leo uwanja wa ndege kuupokea mwili wa Zulu ni Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na waumini wa Kituo cha Maombezi cha Marian Ubungo, wakiongozwa na Padri Felician Nkwera.
 
 Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu ambaye hakuwa tayari kutaja jina gazetini , Zulu alikutwa  damu zikimtoka sehemu ya kichwa na kuegama mezani akiwa ameshika msalaba na picha ya Bikira Maria vilivyokuwa chumbani.
Awali, taarifa ya Katibu huyo kuhusu kifo hicho, iliyotolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Dodoma ilieleza kuwa Zulu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kichwa kwa muda mrefu.
 
Zulu aliyeacha mjane na watoto wanne, Philomena, Maria Emmaculate, Felistas na Augustina,  alikuwa nchini Malaysia, akisoma Shahada ya kwanza ya Mawasiliano na Usimamizi wa Vyombo vya Habari katika Chuo Kikuu cha Taylor tangu Julai 2010, na alitarajiwa kumaliza masomo yake Julai, mwaka huu.
Alizaliwa Julai 10 mwaka 1957 huko Songea. 
 
Alipata elimu ya msingi na sekondari Songea kabla ya kusomea uandishi wa habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari (TSJ) (sasa SJMC-UDSM) jijini Dar es Salaam.
 
Aliwahi kufanyakazi katika Shirika la Utangazaji la Tanzania (RTD) sasa TBC Taifa mwaka 1976 kama Mwandishi wa Habari Msaidizi na hatimaye kupandishwa cheo kuwa Mwandishi wa Habari kabla ya kuhamia Shirika la Magazeti la Chama (Uhuru na Mzalendo) kama Mwandishi Mwandamizi mwaka 1985. 

Mwaka 1986 hadi 1987 alipata fursa ya kusomea masomo ya Uandishi wa Habari ya Kimataifa huko nchini Urusi. Mwaka 1991 aliajiriwa kama Mhariri Msaidizi katika gazeti la The Express kabla ya kujiunga na Sauti ya Ujerumani ambapo alifanya kazi kama Mwandishi Mwandamizi kuanzia mwaka 1995.
 
Aliajiriwa na Bunge mwaka 1998 kwa cheo cha Ofisa Habari Mwandamizi, mpaka mauti inamkuta alikuwa Afisa Habari Mkuu Daraja la Pili.
via: jumamtanda blog

Wednesday, May 29, 2013

UHABA WA VYOO SHULENI KIKWAZO KINGINE KATIKA KUBORESHA ELIMU

Mkuu wa Shule ya Sekondari Londoni, Mwl. Chris Mwageni (katikati) akihojiwa na waandishi wa habari wa Jogoo FM Aden Mbele aliyeshika kinasa sauti na Tamimu Adamu ( kushoto) wakifuatilia nini kiini cha tatizo la vyoo katika shule za msingi, Sekondari vyuo na pengine hata sehemu za kazi. Mahojiano hayo yalifanyika Ofisi za Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini, Uwaqnja wa sabasaba-Matarawe Songea jana.
Na Mwandishi wetu.
UHABA wa vyoo katika shule za msingi, sekondari na hata vyuo mbalimbali hapa nchini ni kikwazo kingine cha kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Marafiki wa Elimu Songea, Bw. Juma Nyumayo, wakati akihojiwa na Redio Jogoo FM ya mkoani Ruvuma.
Bw. Nyumayo amesema takwimu zinaonyesha kuna uhaba mkubwa wa choo shuleni na wakati huohuo katika majengo yaliyokamilika katika Shule za sekondari au vyuo miundombinu yake kuharibiwa kwa makusudi au kutokuwa na elimu ya kuvitumia vyoo hivyo.
"Mfano kwenye baadhi ya  shule au vyuo vya elimu ya juu wanakotumia vyoo vya kisasa miundombinu yake imeharibiwa na kusababisha adha kubwa," amefafanua kuwa hiyo ni kwasababu ya kukosa mafunzo yanayozingatiwa na watumiaji wa vyoo hivyo.
Akizungumzia shule za msingi ambako kuna baadhi ya Shule kutokuwa na choo kabisa au walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja, Mwenyekiti Nyumayo amesema hilo ni tatizo linalowakabili wadau wa elimu kutohakikisha ujenzi kulingana na sera na kuweka choo kama kitu kidogo katika shule.
"Hapa ni uzoefu tunaoupata kuwa hata baadhi ya nyumba katika jamii zetu hazina vyoo, hivyo jamii inaona hata shule hazina umuhimu wa kujengewa choo," alisema.
Alifafanua kuwa hata shule za vyoo, vyoo vyake ni vichafu au vimejaa na wadau wa elimu hawachukuwi hatua.
"Sisi kama marafiki wa elimu mkoani hapa tunaomba kuangalia upya namna ya kuboresha vyoo na view safi muda wote ili kupafanya shuleni mahali bora pa kuishi walimu na wanafunzi, kuliko ilivyosasa," alisema Bw. Nyumayo.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Londoni yenye kidato cha I-VI,  Mwl. Christopher Mwageni, amesema yeye anaishukuru serikali na jumuia ya shule yake kwa kuvijenga vyoo vya kutosha katika shule hiyo.
Mwl. Mwageni alisema kutokana na changamoto ya choo wanafunzi wake hupewa mafunzo ya namna ya kutumia choo na maarifa hayo kuhamishia nyumbani kwao.
Amesema walimu na wanafunzi wanaotumia choo kimoja huathirika kisaikolojia na kuharibu mfumo mzima wa kufunisha na kujifunza.
"Mwalimu anayelazimika kuvizia kwenda choo cha wanafunzi na wanafunzi wanaovizia kwenda choo anachotumia mwalimu huathirika kisaikolojia," alisisitiza Mwl. Mwageni.
Kwaujumla wadau hao wote wawili wameomba serikali za mitaa na vijiji kusimamia ujenzi wa vyoo katika shule zao.
Mwisho

TASWIRA YA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI

Picture 

Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk Emmanuel Nchimbi akielekea kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka askari wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.
Picture
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akitoa heshima zake mara baada ya kuweka shada la maua.
Picture
Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani kutoka Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu.

Tanzania imesema shughuli ya operesheni za kulinda amani katika mataifa yenye mvutano wa kivita barani Afrika zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upelekwaji wa wanajeshi na udhibiti wa rasilimali na utoaji wa maamuzi.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar e s Salaam, mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Dk
Emmanuel Nchimbi amesema tunapoadhimisha siku hii pia tunawakumbuka raia, askari na wapiganaji zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha tangu mwaka 1948 wakiwa katika zoezi la kulinda amani.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alberic Kacou amepongeza vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania na Polisi wa Usalama wa Raia kwa kuandaa tukio hilo la kumbukumbu ya walinda amani wa Umoja wa mataifa wake kwa waume waliopoteza maisha yao.

Amesema katika siku hii ya kimataifa, tuitumie kuwakumbuka walinda amani zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha na kuwaunga mkono askari zaidi ya 111,000 waliopo na wanaoendelea kulinda amani katika nchi mbalimbali zilizo na migogoro.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye Mnara wa Mashujaa viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja viongozi wa dini. (Picha na Dewji Blog).


Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiwasili kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam kushiriki kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.


Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi, Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan na Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwa wimbo wa mataifa kwenye maadhimisho hayo.


Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.

Mgeni rasmi Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara huo.


Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akielekea kuweka shada la maua kwenye maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.


Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiweka shada la maua kwenye mnara huo.


Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa kwa niaba ya Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka Askari wa kulinda Amani wa Umoja wa mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.


Mmoja wa askari wa JWTZ akipendisha bendera ya Umoja wa Mataifa kama ishara ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja huo wanaolinda Amani katika nchi mbalimbali za Afrika.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya kuwakumba Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.


Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Kazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dk. Alberic Kacou kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.


Zainab Abdallah moja ya Vilabu vya Umoja wa Mataifa akighani shairi wakati wa maadhimisho hayo.


Baadhi ya Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.


Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania Bw.George Otoo (wa pili kulia) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (kulia) wakiwa na baadhi ya maafisa mbalimbali wa jeshi la Tanzania wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho hayo.


Kushoto ni Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na baadhi ya mabalozi na maafisa mbalimbali wa jeshi nchini.


Baadhi ya Askari Wanawake wa Vikosi vya Kulinda Usalama wa Tanzania wakiimba wimbo maalum wa kuhamasisha Amani katika maadhimisho hayo.


Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akipeana mikono na Askari Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani kutoka Tanzania kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.


Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akisalimiana na Askari wa Kulinda wa Umoja wa Mataifa waliohudhuria maadhisho hayo leo jijini Dar es Salaam.


Wananchi wakitazama yaliyokuwa yakiendelea wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya askari wa kulinda usalama wa Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.


Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akibadilishana mawazo na mmoja wa askari wa Vikosi vya Umoja


via:  http://www.wavuti.com/