Na Juma Nyumayo, Dar
KATIKA hali ya kutia moyo na kuridhishwa kiutendaji, Shirika la Tanzania Mission To tha Poor and Disabled (PADI) lenye makao yake makuu, Mjini Songea mkoa wa Ruvuma limepata Tuzo likiwa ni Mshindi wa kwanza katika kuwahudumia watu hasa wazee na kusukuma mambo ya kisera serikalini.
Kabla ya ugawaji wa Tuzo hizo maelezo yalitolewa na viongozi wa The Foundation for Civil Society, na akaombwa Mgeni rasmi wa hafla hiyo kutoa Tuzo hiyo.
Tuzo hiyo si zwadi kwa Mtendaji Mkuu wa PADI Bw. Iskaka Msigwa na watumishi wenzake bali kwa Mashirika yote ya Mkoa wa Ruvuma, Serikali, wazee wenyewe na watu wote wa Songea ambao wamethibitishiwa kuwa kazi za PADI zimekubalika hapa nchini
Hongera PADI,
Pages
▼
Friday, November 16, 2012
Tamasha la 10 Asasi za kiraia Tanzania 2012 lamalizika
Na Juma Nyumayo, Blue Pearl, Ubungo Plaza--Dar Es Salaam,
Tamasha la siku tatu la asasi za kiraia nchini lililoandaliwa na The Foundation for Civil Society limemalizika jioni hii kwa mafanikio makubwa.
tamasha la Mwaka huu lilikuwa na kauli mbiu ya wajibu wa asasi za kiraia katika mchakato wa kuandika katiba mpya nchini.
Asasi zaidi ya 10 ziliwakilishwa hapa kupitia Mitandao ya wilaya, Mikoa au mashirika miamvuli ambapo washiriki zaidi ya 420 walihudhuria toka mikoa yote ya zamani na iliyoundwa (mipya) toka bara na Visiwani.
Maswala kadhaa yamejadiliwa mengine yakipatiwa ufumbuzi mengine yakizua mijadala ya kitaifa lakini kubwa ni kulenga kupata katiba nzuri itakayotokana na mawazo na mahitaji halisi ya watanzania wenyewe.
Sintofahamu iliwakuimba wajumbe baada ya wasomi waliobobea katika nyanja za kisheria walipogusa kuwa KATIBA wanayoitaka ni ya nchi gani? kwakuiwa mpaka sasa Muungano wetu una nyufa kadhaa, wakati ambapo Wazanzibari wana Katiba yao, nchi yao na watu wa bara hawana Tanganyika yao> Hivyo suala la Muungano limetakiwa kujadiliwa na kupatiwa muafaka.