Pages

Friday, August 27, 2010

Mkuu wa Mkoa Dkt Ishengoma ashangazwa na viroba!

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma (aliyekaa) akipokea mkono wa Pongezi toka kwa Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Mkoani Ruvuma ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya UTPC na Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo na Maadili wa Umoja huo Tanzania Ofisini kwake mjini Songea hivi karibuni. Dkt Ishengoma alishinda katika kinyang'anyiro cha kura za maoni CCM Viti maalum wanawake Mkoa wa Morogoro. (Picha na Muhidin Amri) Picha ya Pili ni Mjasiliamali akiwa amebeba miwa kichwani akitafuta wateja katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani katika eneo la Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma hivi karibuni (picha na Muhidin Amri), Picha ya tatu Mkuu w\a Mkoa wa Ruvuma dkt Christine Ishengoma akipokea maelezo toka kwa Meneja wa Wakala wa hifadhi ya Chakula Taifa (NFRA) Richard Mulokozi baada ya kushangazwa kuona mahindi yanahifadhiwa kwenye viroba badala ya magunia. Mavuno ya mahaindi yameongezeka maradufu mkoani hapa hasa kwajili ya usimamizi imara na matumizi mazuri ya mbolea ya ruzuku msimu huu ambapo mkoa ulitumia Pembejeo za zaidi ya Shilingi Bilioni 10.6. (Picha na Muhidin Amri maelezo yote na Juma Nyumayo)





Wanafunzi toka UDSM wakitambulishwa RUNECISO!

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Fatuma S. Lazaro, (katikati) na Elizabeth C. Mbena , wakipatiwa maelekezo kutoka kwa Katibu wa mtandao wa asasi zisizo za kiserikali mkoa wa Ruvuma (RUNECISO) , Juma Nyumayo, (Picha ya 1&2) Picha ya 3 wakiwa wanatambulishwa kwenye Ofisi jirani ya SACCOS ya walimu Songea vijijini mkoani Ruvuma (Picha na Ndolanga, maelezo na Fatuma S. Lazaro)





Wednesday, August 25, 2010

Mhe. Manyanya (MNEC) katika sura tofauti!



Mhe. Manyanya akiwa katika sura tofauti mara baada ya uzinduzi wa kampeni za CCM kitaifa katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi, Agosti 22, 2010. alikuwa akizungumzia hasa umuhimu wa mgombea Urais Mhe Jakaya Kikwete na mgombea Mwenza wake Dkt. Ghalib Bilal kuwa watashinda kwa kishindo na kwamba CCM imetekeleza mabo mengi katika Ilani yake ya uchaguzi ya Mwaka 2005. Hilo gari la Kijani ni la Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Mhe. Jakaya Kikwete, akiondoka katika Viwanja hivyo wananchi, wakereketwa na wapenzi wa CCM wakimpungia na kumtakia heri katika safari yake ya kampeni itakayochukua umbali wa takriban km 38,000 ardhini nchi nzima. (Picha zote na Maelezo na Juma Nyumayo)







Mwenyekiti Ruvuma Press akiwa Jangwani-Dar


Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club, Juma Nyumayo, alipohudhuria uzinduzi wa kampeni za kitaifa za CCM Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam. Mlezi wa Chama hicho Mhe. Eng. Stella Manyanya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) pia alikuwepo na ndiye aliyemshauri Mwenyekiti huyo awepo siku hiyo.(Picha na Credo Driver wa Mhe. Manyanya)

Tuesday, August 24, 2010

POWER TILLER BWANA, KIBOKO!



  1. Power Tiller, ikishamaliza kulima, unaitwisha mahindi katika tela hapo nyuma, likishafika nyumbani unafunga kinu cha kupukuchua, halafu kinu cha kusaga litume kazi upendavyo kuhakikisha unafanikisha Mpango wa kilimo Kwanza.
  2. Hapa Power Tiller lipomzigoni kama lilivyopigwa picha na Mpigapicha wetu linapukuchua mahindi eneo la Madaba Songea vijijini. (Picha na Juma Nyumayo)

Wanachama wa Ruvuma Press wakiwa kazini


Baadhi ya wanachama wa Ruvuma Press Club wakiwa kazini ndani ya ofisi ya kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Ruvuma, Bw. David Masiko,(hayupo pichani) Mstari wa mbele toka kushoto ni Emmanuel Msigwa wa Majira, Editha Karlo wa Mtanzania na Juma Nyumayo wa Habarileo. waandishi hao walitaka kujua ukweli kuhusu baadhi magazeti kuandika kukamatwa kwa Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya (Mb) na wapambe wake kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni za CCM mkoani hapa. Jambo hilo lilipingwa vikali na Taasisi hiyo na kusisitiza kuwa waandishi hao waliipotosha jamii kwakuwa wao hawakumkamata isipokuwa walimuita kwa mahojiano. Mhe. Manyanya ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa (MNEC) ni mlezi wa Ruvuma Press Club pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Jamhuri iliyoshughulikia uchunguzi wa RICHMOND.

Waandishi Ruvuma wakifuatilia jambo


Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club, Juma Nyumayo, (Kushoto) na Katibu Msaidizi wa Ruvuma Press Club, Nathan Mtega, wakifuatilia mashindano ya warembo katika viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa vita vya Majimaji Manispaa ya Songea.

VIONGOZI RUVUMA PRESS


Viongozi wa Ruvuma Press Club (kutoka kushoto) Mtunza Hazina, Jacquline Clavery Moyo, Mwenyekiti Juma Nyumayo wakimwelekeza jambo Mwandishi wa gazeti la Mtanzania Editha Karlo jambo la kurekebisha wakati Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma Deogratias Ponera anayefanya mafunzo kwa vitendo kwenye chama hicho akiangalia. (Picha na Agustino Chindiye)

Friday, August 13, 2010

WANAHABARI WANAPOKUTANA NA TAKUKURU

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma Daudi Masiko, (Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma kuhusiana na baadhi ya wanasiasa walioshikiliwa kufuatia tuhuma za rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni CCM mkoani Ruvuma. wengine katikati ni Mwanasheria na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU mkoa Maria Mwakatobe na Bertha madilu Naibu Afisa Elimu kwa Umma Takukuru Mkoa wa Ruvuma.
Kikao hiocho kiliitishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Juma Nyumayo kwa lengo la kuwekana sawa katika namna ya utoaji wa taarifa vitendo vya rushwa kutoka taasisi hiyo mkoani hapa na kupata ufafanuzi kuhusu mchakato wa kura za maoni ziloivyoendeshwa na wale waliotuhumiwa na vitendo vya kutoa au kupokea rushwa katika kusaka madaraka.
(Picha na Muhidin Amri--Ndolanga)