Pages

Saturday, February 27, 2010

Magereza Kitai.

Hili ni Shamba la kuzalisha Mbegu la Gereza la Kitai, Mbinga.
Hivi karibuni Shamba hilo lilitembelewa na Makamu wa Rais, Dkt Ali Mohamed Shein, ambaye alisifu juhudi za kazi za Kilimo hasa kuzalisha mbegu za Mahindi bora ili kuwauzia wakulima wazalishe zaidi kwa usalama wa chakula. (Picha na Juma Nyumayo)

Hayo ya Songea Mjini

Wananchi wakifuatilia maandalizi ya maadhimisho ya Mashujaa wa Vita Vya Majimaji, katika Makumbusho yaliyopandishwa hadhi kuwa ya Kitaifa eneo la Mahenge, Mjini Songea. Hapa wanamsubiri Makamu wa Rais Dkt. Ali Mohamed Shein, aliyetembelea makumbusho hayo hivi karibuni. (Picha Kwa hisani ya Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club, Juma Nyumayo)

Ruvuma Daima Inavuma

KIHISTORIA mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa ambayo inatakiwa kuenziwa kutokana na hali halisi ya mapambano dhidi ya ukoloni.