Na Steven Augustino, Tunduru
 
VYOMBO vya Habari nchini vimehimizwa kufuatilia na kuandika Habari za maendeleo, Changamoto na matatizo yote yanayo vikabiri Vijiji na Wilaya zilizopo pembezoni .
 
Haya yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho wakati akitoa taarifa ya Utekeelezaji wa Serikali ya awamu ya  Nne kupitia ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2005 /2012.
 
Aidha katika taarifa hiyo Dc, Nalicho alidai kuwa endapo daraja la Vyombo vya Habari na wanahabari hawatatembelea na kuandika taarifa hizo watakuwa hawawatendei haki wananchi wa maeneo hayo hali ambayo itawafanya waendelee kulishwa taarifa na matukio yanayo patikana mijini pekee.
 
Akifafanua taarifa hiyo Dc, Nalicho alisema kuwa mbali na Juhudi za Serikali kupeleka Maendeleo kupitia Sekta mbalimbali katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, bado taarifa zake zimekuwa haziandikwi vyakutosha ikiliganishwa na maeneo mengine.
 
Alisema Wilaya hiyo ambayo ipo Pembezoni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za kutokuwa na Barabara za uhakika zinazo unganisha makao makuu ya Wilaya hiyo na Mkoa wa Ruvuma mjini Songea na Wilaya ya Tunduru na Nanyumbo Mkoani Mtwara hali ambayo imezusha malalamiko mengi hasa nyakaati za masika.
 
Akizungumzia mapato ya ndani katika halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Nalicho alisema kuwa katika kipindi hicho Halmashauri ya Wilaya hiyo imefanikiwa kuongeza hadi kufikia Tsh.718, 018,977 .43 kutoka Tsh. 201,738,593.78 mwaka 2005 ilikuwa ni ongezeko la kiasi cha Tsh. 516,280,393.65.
 
Kuhusu Sekta ya Uzalishaji wa Mazao mbali mbali ya Chakula Dc, Nalicho alisema kuwa  katika kipindi hicho Wilaya imeongeza kutoka tani 115,199 hadi tani 328,424 likiwa ni ongezeko la asilimia 169%.
 
Alisema hali hiyo imetokana na Wilaya hiyo kuboresha miundo mbinu ya kujenga mifereji ya Umwagiliaji. Kupeleka Matrekta makubwa  25 kutoka 0 mwaka 2005, Materekta madogo Powertillers 187 na pembejeo za Kilimo kutoka tani 900.65 mwaka 2005  hadi tani 6,412 mwak 2012.
 
Alisema upande wa Sekta ya Mifugo Dc, Nalicho alisema kuwa Wilaya hiyo imepiga hatua kwa kuwa na ongezeko la Ng`ombe 35,758 kutoka 2,780 mwaka 2005, Mbuzi 43,413 kutoka 18,700, Nguruwe 3,110 kutoka 406 na Kuku 310,900 kutoka 107,430 hali ambayo    imewasaidia wananchi wa Wilaya hiyokuinua vipato vyao.
 
Akizungumzia changamoto mbalimbali na Mikakati yake Bw. Nalicho alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa vikwazo hivyo Wilaya yake imekuwa ikijitahidi kukabiliana navyo ikiwa ni pamoja na kuandaa Sheria ndogo ndogo za kukabiliana navyo.