Monday, March 26, 2012

Kwanini watu huharibu kumbukumbu?

Barabara Dar kwenda Morogoro eneo la Ubungo linavyoonekana baada ya kupanuliwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.


Miaka ya 1995 hadi 2005 Serikali ya awamu ya tatu Waziri Mkuu wakati ule Mheshimiwa Frederick Sumaye chini ya Rais Che Ben Mkapa alifanya maamuzi ambayo hayatasahaulika, kwanza alilivunja Baraza la madiwani wa Jiji la Dar es Salaam akaunda Tume ya Jiji la Dar es Salaa, ikaongozwa na Bw. Keenja Tume ile ilifanya kazi nzuri saana. Pili akaamuru kuvunjwa kwa nyumba zilizopo kandokando ya barabar ya Morogoro tokea pale ubungo kuelekea Kimara kupisha uapanuzi wa barabara hiyo ili Foleni kubwa ya magari ipungue katika hicho kibarabara kimoja na kuwa mbili za kuingia mbili zinatoa. mheshimiwa benjamin Mkapa aliifungua barabara ile mimi nilikuwepo pale Ubungo Minazi karibu na Jengo la Tanesco. Mkapa aliifungua barabara ile pamoja na Kituo kile cha mabasi ya Daladala kwa Mbwembwe kibao akiongozwa na maneno ya uhakika ya kuitunza barabara ile na Dkt. John Pombe Magufuli waziri wake aliyekuwa akiwaita Askari wa mwamvuli pamoja na viongozi wengine kibao wa ndani na nje hasa wale walifadhili ujenzi wa barabara ile. Cha kushangaza leo nimezuru eneo lile na kile kibao kilichoandikwa Tarehe ya ufunguzi kimeng'olewa. Hakuna anayejali. Tabia hii ipo kila mahala sasa. kumbukumbu zapotezwa kwaajili au ya biashara ya chuma chakavu au ni ujinga tu? kwa wale wanaojali historia tabia hii inachukiza sana.

Saturday, March 24, 2012

Kama naanza vile!



Ndugu wapendwa ni kitambo sijawapatia vile vitu mwavitaka. Hii ilitokana na matatizo ya hapa na pale ya ki- technolojia lakini nimekwisha weka mambo sawasawa.
Nimewakosa sana wasomaji wa nje kama kina Yasinta Ngonyani na Prof. Mbele na wenzao huko majuu na wewe msomaji mpendwa hapo ulipo katika anga za hapa nchini, barani Afrika, Asia, Ulaya, Marekani na kwengineko. Naahidi kufanya mabadiliko makubwa tuombeane uzima.