Monday, March 29, 2010

Katibu Mtendaji TACOSODE anaposisitiza jambo!

Katibu Mtendaji wa Tanzania Council for Social Development (Tacosode) amesema ni muhimu kwa wananchi na serikali zao kushirikiana kwa karibu katika kufuatilia Rasilimali za Umma kwa maendeleo.
hayo ameyasema katika Ukumbi wa VETA Mjini Songea wakati akifungua mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii wa kufuatilia matumizi ya fedha za umma katika Manispaa ya Songea, Wilaya za Namtumbo, Songea vijijini , Mbinga na Tunduru.
Bibi Kapinga amesema ni jukumu la watu kuhakikisha wanafuatilia mipango na utekelezaji wa shughuli zote kwa njia shirikishi kwani maendeleo ya kiuchumi na kijamii hayatafikiwa iwapo wananchi hawatajua namna ya rasilimali zao zinavyotumika na ushiriki ulivyo.
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na mada mbalimbali wanazojifunza wamevutiwa sana uamuzi wa Baraza la vyama vya Hiari na Maendeleo ya Jamii TACOSODE kwa uamuzi wa kuendesha mafunzo hayo mkoani Ruvuma kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society.
Akielezea umuhimu wa uamuzi huo kwaniaba ya wakazi wa Ruvuma, Katibu wa Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali wilaya ya Songea SONNGo Bw. Mathew Ngalimanayo alisema Tacosode imechukua uamuzi ambao AZIse nyingi hazijawahi kuthubutu "Tacosode wameanza kuonyesha njia, tunaomba pia mashirika mengine yafuate nyayo ili kuharakisha maendeleo mikoa ya pembezoni," alisema na kumpongezaKatibu Mtendaji Theofrida Kapinga kwa kutoa wito kwa wanaRuvuma kujenga mahoteli mazuri kwaajili ya wageni.
Alifikia hatua hiyo kwakuwa wageni ndio huleta chachu ya maendeleo katika maeneo husika.

RUVUMA WAJENGEWA UWEZO KUFUATILIA FEDHA ZA UMMA


Washiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii kufuatilia Matumizi ya Fedha za Umma wakiwa wanafuatilia hotuba ya katibu Mtendaji wa TACOSODE wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea Ukumbi wa VETA Manispaa ya Songea kwa Siku tano.(Picha na Juma Nyumayo)

Wednesday, March 24, 2010

Maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani Ruvuma

Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani Mkoani Ruvuma yamefanyika Mtaa wa Ruvuma Chini Manispaa ya Songea, Pichani wananchi wakiwa katika msururu wa kupima afya yao hasa VVU/UKIMWI Mgeni rasmi wa Siku hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea, Thomas Ole Sabaya (Picha na Juma Nyumayo)

Picha ya pili ni Askari wa Kikosi cha 401 KV akiwa tayari kwa kazi iliyoko mbele yake na kuitekeleza kikamilifu. wananchi wametakiwa kuwa kama askari kupambana na magonjwa kama Kifua Kikuu kwa kasi na Mbinu mpya ili kuutokomeza. (Picha na Juma Nyumayo)



Monday, March 15, 2010

Mambo ya Mkataba Souwasa!

Mkurugenzi wa Souwasa, Mhandisi Fransis Kapongo na Mhandisi Laurent Sechu wa Don Consult Ltd wakibadirishana vitabu vya Mkataba wakiangaliwa na Mwenyekiti wqa SOUWASA Adrian Komba (Kushoto) na Mkurugenzi wa Sajdi & Partners Izzat Sajdi toka Jordan (kulia) Shrehe hiyo ilihudhuriwa na Viongozi wa mamlaka za maji, Viongozi wa Serikali, Waheshimiwa Wabunge na Wakuu wa Wilaya toka wilaya za Songea, Mbinga, Namtumbo na Tunduru. Wahandisi washauri hao watafanya kazi ya kuandaa namna ya kuboresha upatikanaji wa maji katika miji hiyo midogo na Kuboresha Mtandao wa maji Safi na Taka Manispaa ya Songea, kwa Muda wa miezi 12 kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2. ambapo watatafutwa wakandarasi kwaajili ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa Muda wa Miezi 18. Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk Christine Ishengoma amewalaumu wananchi wa Manispaa ya Songea kutochangamkia fursa ya kutumia Mtandao wa maji safi na Taka uliopita kwenye maeneo yao.

Thursday, March 11, 2010

Mambo ya Mganda hayo!


Ngoma ya Mganda kutoka Kata ya kilagano, wakionyesha manjonjo yao kwa utaalamu wa kupiga ngoma, kupuliza mapenenga na kuimba kwa 'step', Step yako weweee! One, Two, .......Ndo mambo ya Songea. (Picha na Juma Nyumayo)

Thursday, March 4, 2010

Mafunzo ya Dhana ya Jinsia TGNP


Mwezeshaji toka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Beatrice Ezakiel, akisisitiza jambo huku Mwezeshaji mwenza Gloria wa TGNP akimwangalia wakati wa kuwakilisha mada kwa waandishi wa habari, wasanii na Wachora Vibonzo magazetini kuhusu mapinduzi ya Kijinsia na Vugvugu la kumkomboa mwanamke.
(Picha na Juma Nyumayo)

Uchaguzi wa Dar City Press Club



Hawa ni baadhi ya wanachama wa DCPC wakiwa na furaha mara baada ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ambao uliweka historia ya Hamsini kwa hamsini (Fifty Fifty). Mkutano huo wa Uchaguzi Ulifanywa katika Ukumbi wa Habari Maelezo (Kama unavyouona kwa nje hapo pichani) Michael Chatta alichaguliwa kwa kura nyingi kuwa Mwenyekiti kwa kipindi cha miaka mitano. Nafasi yaMakamu Mwenyekiti imechukuliwa na Benjamin Masese.
Katibu Mkuu ni, Milan Divecha wakati Betty Tesha amechaguliwa kuwa Katibu Msaidizi. Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTPC, Lucy Ogutu, ameaminiwa na Kupewa nafasi ya Mweka Hazina akisaidiwa na Erodia Petter.
Wajumbe: Jane Mihanji na Beatrice Moses walifungana katika kupatakura nyingi na kuongoza kinyang'anyiro hicho. Wengine ni Samson Kamalamo, Salum Mwalimu, Fatma Nyangasa, Judica Tarimo, Abraham Nyantori na Dorice Lawrence.
Mwenyekiti wa Muda wa Uchaguzi huo alikuwa Shadrek Sagati toka habarileo na Msimamizi alikuwa Mjumbe wa Bodi ya UTPC, Bw Juma Nyumayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club.